Thursday, August 11, 2011

10 la maghfira

Assalam Alykum warahmatullah wabarakat.
Namshukuru Allah (s.w) kwa kunifikisha katika Ramadhani ya 11 ikiwa ni siku ya kwanza katika kumi la pili kati ya matatu ya ndani ya Ramadhani.

Tumemaliza kumi la kwanza ambalo ni la rehma na tumelianza kumi la pili la maghfira, hii leo ikiwa ndio swaum ya kwanza ndani ya kumi hili.

Katika kumi hili waumini husamehewa na Allah (s.w) na tumesuniwa na mtume Muhammad (s.a.w) tuzidishe sana katika kuomba msamaha kwa Allah (s.w) huku nasi tukisameheana pale tunapo koseana.

0 comments