Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
(‘Tanzania Commission for
Universities’-TCU) ikishirikiana
na Baraza laTaifa la Elimu ya
Ufundi (‘National Council for
Technical Education’ - NACTE)
pamoja na Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi Elimu ya Juu (Higher
Education Students Loans
Board) inapenda kuutarifu
umma kuhusu utaratibu wa
kujiunga na vyuo vya elimu ya
juu kwa mwaka wa masomo
2012/2013 kupitia mifumo ya
“Pre-entry”, “Mature Age
Entry”, “Equivalent
Qualifications” na mfumo wa
pamoja wa udahili (‘Central
Admission System’) na
utaratibu wa mikopo kama
ifuatavyo:
MFUMO WA UDAHILI KUANZIA
MWAKA 2012/13
1.1 Utaratibu wa Kuendesha
Program za “Pre-entry” na
“Mature Age Entry”
Kuanzia mwaka huu 2012, vyuo
vyote vitakavyotaka kuendesha
mafunzo ya awali kabla ya
mwombaji kustahili kudahiliwa
ili kuweza kujiunga na
programu za elimu ya juu (pre-
entry programmes) pamoja na
kuendesha mitihani ya kupitia
mfumo wa “Mature Age Entry”
vinatakiwa kuwasilisha
programu hizo Tume ya Vyuo
Vikuu (TCU) au Baraza la Taifa la
Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa
uhakiki na kupata kibali.
Programu hizo ni lazima
ziendeshwe kwa muda wa
mwaka mmoja. Hali kadhalika
kwa upande wa mitihani
kupitia mfumo wa mature
entry, Tume kwa ushirikiano na
Baraza, kwa pamoja
wataandaa na kuratibu
utaratibu wa mitihani katika
vituo maalum kikanda ili vyeti
vitakavyotolewa viwe na
ulinganifu unaostahili na
hatimaye kuweza kutumika
katika udahili wa sifa linganishi
katika vyuo mbalimbali.
Vyuo vinatakiwa kuandaa
programu za mifumo ya “Pre-
entry” na “Mature Age Entry”
na kuziwasilisha Tume na
Baraza ili zihakikiwe kwani
mwaka wa masomo kwa
kusudi hili utaanza mwezi
Agosti 2012/2013. Kwa
utaratibu huu, watakaofanya
mafunzo hayo watatakiwa
kufanya mitihani yao na
kujiunga na masomo ya elimu
ya juu katika mwaka wa
masomo 2013/2014.
Kwa taarifa hii, mwaka
2012/13 hakutakuwapo na
udahili wa wanafunzi kwa
mfumo wa “Pre-Entry” na
“Mature Age Entry”.
1.2 Utaratibu wa Udahili Kupitia
Mfumo wa Pamoja (Central
Admission System)
Waombaji watakaopitia mfumo
wa pamoja wa udahili (CAS)
wamegawanyika katika
makundi manne, ambapo
waombaji wa kundi (i), (ii) na
(iii) watatambuliwa kama
“Direct Applicants” na kundi (iv)
watatambuliwa kama “Indirect
Applicants”
Waliohitimu elimu ya sekondari
kidato cha sita katika kipindi
cha miaka miwili iliyopita
pamoja na wale watakaohitimu
mwaka huu.
Waliohitimu mafunzo ya
diploma ya elimu ya ufundi
(NTA level 6) kutoka vyuo
vinavyotambulika na NACTE
miaka miwili iliyopita pamoja
na wale watakaohitimu mwaka
huu;
Waliohitimu mafunzo ya
Diploma ya Ualimu (kutoka
vyuo vinavyotambulika) katika
kipindi cha miaka miwili
iliyopita pamoja na wale
watakaohitimu mwaka huu.
Waombaji ambao sio wa moja
kwa moja (Indirect Applicants)
ni wote waliohitimu kidato cha
sita, Diploma ya Elimu ya Ufundi
(NTA level 6) na Diploma ya
Ualimu katika kipindi cha zaidi
ya miaka miwili iliyopita
(kuanzia 2009 kurudi nyuma).
1.2 Waombaji
Watakaowasilisha Maombi yao
Moja kwa Moja Vyuoni
Waombaji watakaowasilisha
maombi kupitia vyuo husika ni
wenye sifa linganishi
(Equivalent Qualifications) yaani
wenye vyeti vya Astashahada
na Diploma ambazo
hazitambuliwi moja kwa moja
na NACTE. Ili kukamilisha
udahili, wanashauriwa
kuwasiliana na NACTE ili vyeti
vyao vitambuliwe na kusajiliwa
kabla udahili haujaanza.
Vyuo vinavyofundisha
programu mbalimbali katika
ngazi ya Astashahada na
Diploma ambavyo havina usajili
wa NACTE/NECTA vinatakiwa
kuwasilisha matokeo ya
wanafunzi wao NACTE haraka
iwezekanavyo ili matokeo hayo
yaweze kutumika katika
utambuzi wa vyeti vya
wanafunzi husika.
MUDA WA UDAHILI KWA
MAKUNDI MBALIMBALI
Muda wa maombi wa
kuwasilisha maombi ya udahili
kwenye CAS umegawanyika
katika makundi matatu kama
ifuatavyo:
Kundi la Kwanza – (1 Aprili
mpaka 30 Aprili 2012)
Waombaji wote waliomaliza
kidato cha sita, Diploma ya
Elimu ya Ufundi (NTA level 6),
na Diploma ya Ualimu kuanzia
mwaka 2011 kurudi nyuma
wataanza kuomba udahili
kuanzia Aprili 1, 2012 hadi 30
Aprili 2012.
Kundi la Pili
Waombaji wote
watakaomaliza kidato cha sita,
Diploma ya Elimu ya Ufundi na
Diploma ya Ualimu mwaka
2012 wataanza kuomba udahili
baada ya matokeo yao ya
mitihani kutangazwa na
vyombo husika. Hakuna
mwanafunzi atakayesajiliwa
kwa kutumia matokeo ya muda
(provisional or expected
results).
Kundi la Tatu
Waombaji wote ambao ni raia
wa Tanzania waliosoma nje ya
nchi au wenye vyeti ambavyo si
vya mfumo wa elimu ya
Tanzania (mfano: Cambridge,
Bacclaureate, n.k). Waombaji
wa kundi hili wanashauriwa
kuomba udahili mara matokeo
yao yatakapotangazwa na
watatakiwa kupeleka vyeti
vyao Baraza la Taifa la Mitihani
(“National Examinations Council
of Tanzania – NECTA”) au
Baraza la Taifa la Elimu ya
Ufundi (National Council for
Technical Education - NACTE)
kwa ajili ya kulinganisha alama
zao za matokeo au kupata
ithibati kabla ya kuanza
kuomba udahili. Hakuna
wanafunzi watakaodahiliwa
kwa matokeo ya muda.
UTARATIBU WA MIKOPO
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi
wa Elimu ya Juu kwa mamlaka
iliyopewa kisheria itatoa
mwongozo na utaratibu wa
utoaji wa mikopo mwezi
Februari 2012. Miongozo hii
itachapishwa katika vyombo
vya habari na kusambazwa
kwenye vyuo vyote vya elimu
ya juu nchini na Ofisi za Posta
na kwa Wakuu wa Elimu kila
wilaya. Maombi ya mikopo kwa
mwaka wa masomo 2011/2012
yataanza kupokelewa ifikapo
mwezi Machi 2012 na mwisho
wa kupokea maombi ni tarehe
30 Juni 2012. Utaratibu huu
utahusu waombaji wote wapya
na wale walioko masomoni
katika vyuo vya elimu ya juu.
HITIMISHO
Tunapenda kuwajulisha
waombaji wote kuzingatia
muda wao wa udahili kama
ulivyoainishwa katika tangazo
hili. Muda ukiisha hawataweza
kuomba hadi mwaka wa
masomo 2013/2014. Pia
waombaji wote wanashauriwa
kufuata taratibu za mikopo
kam zitakazotolewa na Bodi ya
Mikopo ili kuepuka usumbufu
unaoweza kujitokeza katika
swala hili
Maelezo zaidi na ufafanuzi
kuhusu udahili na mikopo wa
2012/13 yanapatikana katika
tovuti zifuatazo:
Tume ya Vyuo Vikuu;
www.tcu.go.tz
Baraza la taifa la elimu ya
ufundi; www.nacte.go.tz
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya
Elimu ya Juu; www.heslb.go.tz
IMETOLEWA NA: Katibu
Mtendaji, Tume ya Vyuo Vikuu
Tanzania, S.L.B 6562, Dar es
Salaam. Barua pepe (e-mail)
es@tcu.go.tz
(‘Tanzania Commission for
Universities’-TCU) ikishirikiana
na Baraza laTaifa la Elimu ya
Ufundi (‘National Council for
Technical Education’ - NACTE)
pamoja na Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi Elimu ya Juu (Higher
Education Students Loans
Board) inapenda kuutarifu
umma kuhusu utaratibu wa
kujiunga na vyuo vya elimu ya
juu kwa mwaka wa masomo
2012/2013 kupitia mifumo ya
“Pre-entry”, “Mature Age
Entry”, “Equivalent
Qualifications” na mfumo wa
pamoja wa udahili (‘Central
Admission System’) na
utaratibu wa mikopo kama
ifuatavyo:
MFUMO WA UDAHILI KUANZIA
MWAKA 2012/13
1.1 Utaratibu wa Kuendesha
Program za “Pre-entry” na
“Mature Age Entry”
Kuanzia mwaka huu 2012, vyuo
vyote vitakavyotaka kuendesha
mafunzo ya awali kabla ya
mwombaji kustahili kudahiliwa
ili kuweza kujiunga na
programu za elimu ya juu (pre-
entry programmes) pamoja na
kuendesha mitihani ya kupitia
mfumo wa “Mature Age Entry”
vinatakiwa kuwasilisha
programu hizo Tume ya Vyuo
Vikuu (TCU) au Baraza la Taifa la
Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa
uhakiki na kupata kibali.
Programu hizo ni lazima
ziendeshwe kwa muda wa
mwaka mmoja. Hali kadhalika
kwa upande wa mitihani
kupitia mfumo wa mature
entry, Tume kwa ushirikiano na
Baraza, kwa pamoja
wataandaa na kuratibu
utaratibu wa mitihani katika
vituo maalum kikanda ili vyeti
vitakavyotolewa viwe na
ulinganifu unaostahili na
hatimaye kuweza kutumika
katika udahili wa sifa linganishi
katika vyuo mbalimbali.
Vyuo vinatakiwa kuandaa
programu za mifumo ya “Pre-
entry” na “Mature Age Entry”
na kuziwasilisha Tume na
Baraza ili zihakikiwe kwani
mwaka wa masomo kwa
kusudi hili utaanza mwezi
Agosti 2012/2013. Kwa
utaratibu huu, watakaofanya
mafunzo hayo watatakiwa
kufanya mitihani yao na
kujiunga na masomo ya elimu
ya juu katika mwaka wa
masomo 2013/2014.
Kwa taarifa hii, mwaka
2012/13 hakutakuwapo na
udahili wa wanafunzi kwa
mfumo wa “Pre-Entry” na
“Mature Age Entry”.
1.2 Utaratibu wa Udahili Kupitia
Mfumo wa Pamoja (Central
Admission System)
Waombaji watakaopitia mfumo
wa pamoja wa udahili (CAS)
wamegawanyika katika
makundi manne, ambapo
waombaji wa kundi (i), (ii) na
(iii) watatambuliwa kama
“Direct Applicants” na kundi (iv)
watatambuliwa kama “Indirect
Applicants”
Waliohitimu elimu ya sekondari
kidato cha sita katika kipindi
cha miaka miwili iliyopita
pamoja na wale watakaohitimu
mwaka huu.
Waliohitimu mafunzo ya
diploma ya elimu ya ufundi
(NTA level 6) kutoka vyuo
vinavyotambulika na NACTE
miaka miwili iliyopita pamoja
na wale watakaohitimu mwaka
huu;
Waliohitimu mafunzo ya
Diploma ya Ualimu (kutoka
vyuo vinavyotambulika) katika
kipindi cha miaka miwili
iliyopita pamoja na wale
watakaohitimu mwaka huu.
Waombaji ambao sio wa moja
kwa moja (Indirect Applicants)
ni wote waliohitimu kidato cha
sita, Diploma ya Elimu ya Ufundi
(NTA level 6) na Diploma ya
Ualimu katika kipindi cha zaidi
ya miaka miwili iliyopita
(kuanzia 2009 kurudi nyuma).
1.2 Waombaji
Watakaowasilisha Maombi yao
Moja kwa Moja Vyuoni
Waombaji watakaowasilisha
maombi kupitia vyuo husika ni
wenye sifa linganishi
(Equivalent Qualifications) yaani
wenye vyeti vya Astashahada
na Diploma ambazo
hazitambuliwi moja kwa moja
na NACTE. Ili kukamilisha
udahili, wanashauriwa
kuwasiliana na NACTE ili vyeti
vyao vitambuliwe na kusajiliwa
kabla udahili haujaanza.
Vyuo vinavyofundisha
programu mbalimbali katika
ngazi ya Astashahada na
Diploma ambavyo havina usajili
wa NACTE/NECTA vinatakiwa
kuwasilisha matokeo ya
wanafunzi wao NACTE haraka
iwezekanavyo ili matokeo hayo
yaweze kutumika katika
utambuzi wa vyeti vya
wanafunzi husika.
MUDA WA UDAHILI KWA
MAKUNDI MBALIMBALI
Muda wa maombi wa
kuwasilisha maombi ya udahili
kwenye CAS umegawanyika
katika makundi matatu kama
ifuatavyo:
Kundi la Kwanza – (1 Aprili
mpaka 30 Aprili 2012)
Waombaji wote waliomaliza
kidato cha sita, Diploma ya
Elimu ya Ufundi (NTA level 6),
na Diploma ya Ualimu kuanzia
mwaka 2011 kurudi nyuma
wataanza kuomba udahili
kuanzia Aprili 1, 2012 hadi 30
Aprili 2012.
Kundi la Pili
Waombaji wote
watakaomaliza kidato cha sita,
Diploma ya Elimu ya Ufundi na
Diploma ya Ualimu mwaka
2012 wataanza kuomba udahili
baada ya matokeo yao ya
mitihani kutangazwa na
vyombo husika. Hakuna
mwanafunzi atakayesajiliwa
kwa kutumia matokeo ya muda
(provisional or expected
results).
Kundi la Tatu
Waombaji wote ambao ni raia
wa Tanzania waliosoma nje ya
nchi au wenye vyeti ambavyo si
vya mfumo wa elimu ya
Tanzania (mfano: Cambridge,
Bacclaureate, n.k). Waombaji
wa kundi hili wanashauriwa
kuomba udahili mara matokeo
yao yatakapotangazwa na
watatakiwa kupeleka vyeti
vyao Baraza la Taifa la Mitihani
(“National Examinations Council
of Tanzania – NECTA”) au
Baraza la Taifa la Elimu ya
Ufundi (National Council for
Technical Education - NACTE)
kwa ajili ya kulinganisha alama
zao za matokeo au kupata
ithibati kabla ya kuanza
kuomba udahili. Hakuna
wanafunzi watakaodahiliwa
kwa matokeo ya muda.
UTARATIBU WA MIKOPO
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi
wa Elimu ya Juu kwa mamlaka
iliyopewa kisheria itatoa
mwongozo na utaratibu wa
utoaji wa mikopo mwezi
Februari 2012. Miongozo hii
itachapishwa katika vyombo
vya habari na kusambazwa
kwenye vyuo vyote vya elimu
ya juu nchini na Ofisi za Posta
na kwa Wakuu wa Elimu kila
wilaya. Maombi ya mikopo kwa
mwaka wa masomo 2011/2012
yataanza kupokelewa ifikapo
mwezi Machi 2012 na mwisho
wa kupokea maombi ni tarehe
30 Juni 2012. Utaratibu huu
utahusu waombaji wote wapya
na wale walioko masomoni
katika vyuo vya elimu ya juu.
HITIMISHO
Tunapenda kuwajulisha
waombaji wote kuzingatia
muda wao wa udahili kama
ulivyoainishwa katika tangazo
hili. Muda ukiisha hawataweza
kuomba hadi mwaka wa
masomo 2013/2014. Pia
waombaji wote wanashauriwa
kufuata taratibu za mikopo
kam zitakazotolewa na Bodi ya
Mikopo ili kuepuka usumbufu
unaoweza kujitokeza katika
swala hili
Maelezo zaidi na ufafanuzi
kuhusu udahili na mikopo wa
2012/13 yanapatikana katika
tovuti zifuatazo:
Tume ya Vyuo Vikuu;
www.tcu.go.tz
Baraza la taifa la elimu ya
ufundi; www.nacte.go.tz
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya
Elimu ya Juu; www.heslb.go.tz
IMETOLEWA NA: Katibu
Mtendaji, Tume ya Vyuo Vikuu
Tanzania, S.L.B 6562, Dar es
Salaam. Barua pepe (e-mail)
es@tcu.go.tz