Sunday, August 10, 2014

TAADHARI KWA WATUMIAJI WA FB:KUWA MAKINI NA KUBADIRISHA RANGI YA FACEBOOK

Watumiaji wa mtandao wa kijamii facebook duniani wametakiwa kuwa makini na tangazo linalowataka kubadilisha rangi ya profile za facebook zao kwani tangazo hilo ni virus.

Mpaka sasa watumia zaidi 10,000 wameshathirika na virus huyo, virus huyo aliwai kutoke hapo awali na akashughulikiwa na mtandao wa facebook lakini mara hii amekuja kivyengine.

Virus huyo huanza kwa mundo wa tangazo la applicaton (app) ambayo linamwambia mtumia facebook kuwa anaweza kubadilisha rangi ya theme ya profile yake, anapofungua kiunganishi hicho humtaka mtumiaji huyo kudownload app hiyo, na anapofanya hivyo hupelekwe moja kwa moja katika mitandao feki ijulikano ama malicious phishing site.

Mtumiaj wa facebook anapokamilisha hatua hizo anakuwa hatari kwani wezi wa mitandao wanaweza kuifikia password yake facebook na kuwa rahisi kuhujumiwa kupitia anuani yake ya facebook.

0 comments