About Us

ABOODMSUNI NETWORK (AN) ni mtandao unasghulikia masuala mbalimbali ya computer, uunganishaji wa network na usimamizi wa shughuli mbalimbali za internet,.

HISTORIA YA ABOODMSUNI NETWORK


ABOODMSUNI NETWORK (AN) ilianza kazi yake katika mwezi wa pili tarehe 21 mwaka 2011 ikiwa inajishughulisha na usimamizi wa blog ya michezo inayokwenda kwa jina la  SPORTS IN BONGO ikiwainafahamika kwa jina la Tanzania Football Event.

Wiki tatu mbele blog ya Aboodmsuni Network ilianza kufanya kazi ikienda kwa jina la TAFAKARI NA BONGE ikiwa ni blog binafsi ya mmiliki wa AN. Blog hii ilivua vazi ya kuwa blog binafsi na kuwa blog ya shughuli zinazo fanywa na AN pamoja na mmiliki wa AN mara baada ya kuanza shughuli ya kutoa huduma ya ukarabati wa computer.

AN ilianza huduma ya ukarabati wa computer mwishoni mwa mwaka 2011 na mwishoni mwa mwaka 2012 ilipata mahali pakufanyia shughuli zake (ofisi) ambapo ipo Mikocheni B jijini Dar es salaam.

MMILIKI WA ABOODMSUNI NETWORK



ABOODMSUNI NETWORK inamilikiwa na Abdallah Hamdun Ibrahim Sulayman ambaye anafahamika kwa majina ya Abood na Msuni yaliyotengeneza Aboodmsuni.

Jina la Abood alipewa na familia yake tangu akiwa mdogo huku jina la Msuni akipewa na Marafiki zake wakati anacheza mpira katika timu ya Miko Boys (Mikovilla) wakati huo ikijulikana kwa jina la 'Watoto Wa Paroko' kutokana na kutumia uwanja wa kanisa Katoliki na kupewa sapoti na kanisa hilo.

Msuni ni mwanafunzi wa Al-Maktoum College Of Engineering and Technology kilichopo Benzi Beach akichukua Bachelor ya Information System and Network Engineering (ISNE).


MAFANIKIO YA AN


AN bado haijafikia hata robo ya malengo iliyojiwekea lakini toka ilipoanza kutoa huduma zake imefanikiwa kupata mafanikio ya fuatayo;

1. Blog ya
SPORTS IN BONGO ilifanikiwa kuwa mshindi wa tatu katika shindano la Best Tanzania Sports Blog 2011, Ikiwa na umri wamiezi sita


2. Blog ya ABOODMSUNI NETWORK ilifanikiwa kuwa mshindi wa pili katika shindano la Best Tanzania Informative Sport Blog 2011, ikiwa na umri wa miezo mitano.


3. Mwezi wa sita mwaka 2011, ABOODMSUNI NETWORK walipewa kazi ya kuandaa na kuiendesha blog ya mashabiki wa Azam FC.

4. Aboodmsuni blogs walipata tuzo toka kwa Azam FC



 

NAMNA YA KUTUFIKIA (CONTACT US)

Email us: aboodmsuni@gmail.com
Call us: +255715602531, +255765578851
Follow us on; Twitter na Facebook