Thursday, June 2, 2011

Imani ya Dini yaleta mtafaruku katika mazishi 2

Kwenye makaburi shughuli iliendelea na mpisha Sophia Salehe aendelee na mkasa.

Kiongozi wa wale vijana akasema Mzee tunataka utuambie maana tumeshapata taarifa zote toka kwa madaktar kuwa huyu maiti alikuwa na upungufu wa damu na madaktar walipokushauri kuwa inabidi aongezewe damu, ukasema haiwezekani wala haruhusu huyu mwanao awekewe damu kwa kuwa imani ya dini yako ya nyie mashahidi wa yehova hairuhusiwi binadamu kuwekewa damu ni dhambi kubwa mno hadi mwanao akakata roho.
Tunataka utuambie kwa nini ulikataa huyu marehemu asiwekewe damu.

Mzee akashika mdomo... Kuonyesha kuwa hawezi kuongea, wale vijana wakaanza kupiga makelele huku wengine wakisema leo amekuwa bubuee... Ataongea tu... Na kama hajibu maswali yetu aondoke na maiti yake akatafute kwa kuzika na sisi shimo letu tunafukia.

Wale vijana wakachukua makoleo na kutishia kuchota udongo kufukia lile shimo Lakini mwenyekiti wa mtaa akawaomba watulie wakati huo nyimbo mbalimbali za kuashiria vurugu ...zingine kama zile za watu wanapokuwa kwenye migomo na maandamano mbalimbali zilitawala.
Ndipo kijana mmoja akasema ''mzee inabidi achapwe viboko kumi hapahapa .... Vijana wote walishangilia huku wakipika kelele ndioooooo. Ishu ikaja kuwa nani wa kumchapa yule mzee viboko ingawa pembeni kulikuwa na furushi la fimbo ambalo vijana hao walikuwa wamekuja nalo.....Adhabu hiyo ikawa ngumu kwa kuwa walihofia pale makaburini lolote lingeweza kutokea wakati mzee anakula fimbo.

Kumchapa mzee ikawa ngumu tatizo likawa nani wa kumchapa ikabidi yule kiongozi aseme mzee bwana tunakubadilishia adhabu sawa?
Mzee akasema sawa ....sasa inabidi uingie ndani ya hili kaburi ili umzike mwenyewe kijana wako.

Mzee ikabidi achojoe kivazi cha juu aka koti la suti na viatu na sokx kisha akaingia shimoni... Basi wale jamaa wakamwambia tunakushushia sanduku sanda pokea Wakali chukua sanduku na kuliwekea mle kaburon... mzee akapokea mara tukaskia tiiii..kuashiria kuwa lile sanduku lilimsumbua kisogo katika ushikaji.
Basi bwana baada ya kishindo hiko cha sanduku.... Jamaa wakashangilia sana... Huku wengine wakisema mpeni majani..... Ndio hapo wale vijana wakaanza kumpati a majani...fito, vibao.... Kama ilivyokawaida wakat wa zoeez la uzikaji kuna baadhi ya vifaa huingia kabla udongo haujaanza kutupiwa mle ndani.. ..mzee ikabidi afanye hiyo kazi kwa mujibu wa maelekezo aliyopewa akiwa chini ya usimamizi mkali.

Mzee alimaliza zoezi hilo na vijana waka mwambia atoke mle ndani, mzee akatoka akiwa vumbi tupu.. Cha kushangaza akiwa ametoka aliongea kwa sauti kuwa OooYeshu ameniongoza ...akimaanisha Anapata mateso kama aliyopata Yesu toka kwa wayahudi...lakin wale jamaa walimpuuza na kumsihi aache kelee mzee akatulia.

Akiwa katika hali ile kama mchimbaji mdogo wa madini, wale vijana wakamwambia sasa bado adhabu moja.... Mzee akasema sawa Wakamuamuru aanze kuzika mwenyewe kwa kumalizia zoezi la ufukiaji...ndipo mzee akachukua chepe na kuanza kutupia mchanga mle ndani zoezi lililomchukua takriban dakika ishirini....akiwa ameonekana kuchoka sana huku wale vijana wakiendelea kumuimbia safari hii nyimbo zilibasdilika yakawa mapambio mbalimbali pale msibani huku mda ukiendelea kwenda na giza kuanza kuingia huku baadhi ya watu wakianza kundoka kutokana na zoezi lenyewe kuoneekana kuchukua muda sana kinyume na mazoea ya misiba mingi ambao tuliwahi kuhudhuria wafiwa wakiadhibiwa.

Mzee alifukia takribani nusu ya kaburi ndipo ikabidi wale vijana wamwambie awapishe nao wakashika machepeo na kumalizia kufanya leveling.
Baada ya hapo watu wote waliamuliwa kutoka makaburini huku wakiimba nyimbo mbalimbali za ushindi....

HIVYO NDIVYO SOPHIA SALEH ANAVYO KAMILISHA KUSIMULIA TUKIO LILILO TOKEA IRINGA.

aamsuni

0 comments