Thursday, June 23, 2011

Naomba Muongozo

Nimekuwa sio mfuatiliaji wa karibu wa Bunge na Habari za kitaifa na hivyo kuwa mbali na taratibu za bunge na kushindwa kuelewa bunge linavyoendeshwa.

Jana wakati nasubiri sports extra inayorushwa na clouds fm kulikuwa na kipindi cha top ten za amplifier na tukio la mchangia mada kuhusu madiwani katika bunge lilichukuwa nafasi ya kwanza kwa siku hiyo.

Cha ajabu alipoweka kipengele hicho cha bunge kili ni gea maswali mengi kichwani mwangu ambayo ina ni pelekea ni ombe muongozo kabla sija li chambua bunge letu la sasa.
Kulikuwa na sound track za wabunge chini ya sauti ya mchangia mada kitendo ambacho kilinipelekea kusema wabunge wako sokoni ama katika madarasa ya shule ya msingi.

Ndugu zangu na ombeni Muongozo ni wa taifa letu linapo elekea. Kama katika eneo la kupitisha sheriha ina kelele kuliko madarasa ya wanafunzi wa msingi ina tuonyesha nini.
Hii ni aibu kwa wabunge na Taifa zima, kwa kushindwa kupaheshimu sehemu hizo.

Hapo awali ni lipata kumsikia Spika wa Bunge akilifananisha bunge na soko la Kariakoo namna sauti zinavyo pandizana katika bunge hili.

Naombeni Muongozo niondoe maswali yanayo tawala kichwani mwangu.

0 comments