Wednesday, August 31, 2011

Ujumbe wa Rafiki yangu Semeni. Happy birthday DJ FETTY

Jana kwenye pita pita zangu kwenye mtandao nikiwa nimechoka na shamra shamra za eid pale Jamhuri stadium Morogoro nimekutana na ujumbe wa Rafiki yangu katika mtandao Semeni Nyerere.

"Mwenz umeandama huku mbezi beach cjui kwenu,-kesho guest za kitaa zitafurka, 3bomba ztanunuliwa hadi basi, madada poa watauza knoma kesho, pombe ztanyweka knoma, hjabu kwa heri tena mpaka mfungo ujao, cmu ztapgwa sana kwenda kwa jnsia za kike uko wapi? tukutane ...,kodi bajaji fasta, n.k samahanini cpondei dini ya mtu icpokuwa ndo ukweli wenyewe kama ulikuwa umefunga namumeplan haya hakuna ulchokfanya, ukchukia niblock, but that is the reality," ujumbe wa Semeni Nyerere ndani ya Facebook.

Aliyo yasema rafiki yangu ndiyo yatokeayo kila siku ya Eid napenda kutoa taadhari kwa wale wanaopanga kufanya hivyo hii leo waache kwa sababu zifuatazo.

1. Mtume (s.a.w) anasema yule atakae fanya maovu siku ya eid ni sawa na kufanya maovu siku ya hukumu mbele ya Allah (s.w).

2. Funga yako itakuwa haina faida.
Allah (s.w) anasema katika Qur an tumefaradhishiwa funga ili tuwe wa chamungu (tumuogope Allah (s.w) kwa kuacha makatazo na kuifuata Qur an na Sunna za Mtume (s.a.w)). Kama unafunga na siku unayofungua unafungua na maasi ni kiasi gani Funga haija kuadhiri, zaidi ya kushind njaa.


Mwisho na WATAKIA EID NJEMA WAISLAMU WOTE na vilevile na Watakia Heri ya Kuzaliwa wale Waliozaliwa Leo Akiwemo DJ FETTY, Asnath na wengineo.

0 comments