LEO HII NI SIKU YA TATU TOKEA KUINGIA KWA MWEZI WA DHUL HIJJAH
Anasema mtume wa Allah rehema na amani ziwe juu yake (Hakuna siku ambazo matendo mema ndani yake yanakuwa ni yenye kupendezwa zaidi mbele ya Allah kulikoni Siku hizi (siku kumi za mwezi wa dhul hijja).
Maswahaba wakauliza:Ewe mtume wa Allah, Wala jihadi Kwa ajili ya njia ya Allah?
Akawajibu:Wala jihadi kwa ajili ya njia ya Allah,isipokuwa Kwa yule mtu aliyetoka na nafsi yake na mali zake Kasha kikawa hakijarudi chochote katika hivyo).
JE MATENDO HAYO YANAYO PENDEZWA KUYAFANYA NDANI YA SIKU HIZI NI YAPI???
1:KUFANYA IBADA YA HIJJA NA UMRA:
Kama anavyo tueleza mtume rehema na amani ziwe juu yake: (Ibada ya umra mpaka ibada ya umra ni kifutio cha madhambi Yali kati yake,na ibaada ya hijja iliyo kamilisha nguzo zake na masharti yake Haina malipo isipokuwa pepo)
2:KUFUNGA SIKU HIZI ZOTE TISA AU KADIRI YA UWEZO, KHUSUSANI SIKU YA TISA SIKU YA ARAFA:
Bila shaka ibada ya swaumu ni katika ibaada zenye thawabu mbele ya Allah. Na katika hadithi zilizokuja kuelezea umuhimu na fadhila za swaumu ni hadithi Yake mtume rehema na amani ziwe juu yake: (Mwenye kufunga siku moja kwa ajili ya Allah mwenyezi mungu utauweka uso wake Na moto wa jahanamu muda wa miaka sabini)
Na kuhusiana na fadhila za kufunga siku ya arafa mtume anatueleza ya kwamba: (Funga ya siku ya arafa ninatarajia Allah atawafutia waja madhambi ya mwaka ulio Pita na mwaka ujao)
3:Kuzidisha adhkari mbali mbali katika siku hizi kumi
Kama vile Takbira(ALLAHU AKBARU:Mungu mkumbwa), ALHAMDULILLLAHI:Shukurani zote anastahiki Mwenyezi Mungu.
ISTIGHFARI:Kumtaka msamaha Mwenyezi Mungu. Na mfano wa hizo katika adhkari zilizo pokelewa katika mwongozo wa mtume wetu Muhamadi rehema na amani ziwe juu yake.
4:KUTUBIA KWA ALLAH NA KUJING`OA KUTOKA KATIKA MAASI YOTE.
Kwani utiifu(Kumtii Allah) ni katika sababu za kumfanya mja awe karibu na Allah Na maasi\madhambi ni katika mambo yanayo muweka mja mbali na Allah.
Na toba ni katika mambo yanayo mfurahisha Allah.
5:KUZIDISHA KUFANYA MAMBO YA KHERI.
Kama vile kuswali swala zote kwa nyakati zake. Vile vile kuzidisha ibaada za sunna na kutoa sadaka na kuamrishana mambo mema na Kukatazana maovu nk.
6:KUCHINJA SIKU YA IDI EL ADHHA.
Kwa kumuiga kigezo chetu na mtume wetu nabii Ibrahimu. Na mtume wetu Muhamadi.
Ibada hii ya kuchinja ni ibaada ya sunna, Na wanyama wanao faa kuwachinja ni ngamia, ng`ombe, mbuzi kondoo.
Ngamia au ng`ombe wanaweza changa watu saba, ama mbuzi na kondoo ni kwa mtu mmoja tu.
Mnyama huyu yapaswa asiwe na aibu kama vile uchongo upofu na kilema.
7:KWA MWENYE KUTAKA KUCHINJA NDANI YA SIKU YA IDDI
Basi ni sunna kwa mtu huyu asikate nywele zake na kucha zake.
8:KUJITAHIDI KUSWALI IBADA YA IDI
Kwani ibaada hii kwa mwaka ni mara moja tu,kwa hiyo ni muhimu kujitahidi kutekeleza ibaada hii.



0 comments