Assalam Alaykum Warahmatulla Wabarakatuh.
Namshukuru Mola kwa kunifikisha ijumaa nyingine na kuianza wikiend nyingine. Kama ilivyo ada wengi wetu wikiend ndio wakati muafaka wa kujumuika na familia zetu baada ya kufanya kazi wiki nzima.
Japo kuna baadhi yetu watakuwa kibaruani katika siku hizi za wikiend. Hivyo sina budi kuwatakia IJUMAA KARIM na WIKIEND NJEMA wote na kuwatakia KILA LA KHERI TAIFA STARS hapo jumapili.
UJUMBE WA LEO: KALAMU KARATASI NA UFUTIO
Kijana mmoja baada ya kufunga ndoa, baba yake alimtaka alete kalamu ya risasi karatasi na ufutio. Baada ya kijana huyu kuja na vifaa hivi, baba akamwambia mwanae andika.
Kijana akauliza: Niandike nini?
Baba akamjibu: Andika unacho taka.
Kijana akaandika sentesi.
Baba akamwambia kijana wake: Ifute, akaifuta.
Kisha baba akamwambia kijana wake andika sentesi nyingine.
Yule kijana akaandika sentesi nyingine.
Akamwambia: Ifute, akaifuta.
Kisha akamwambia kwa mara ya tatu: Andika sentesi nyingine.
Kijana akaandika sentesi nyingine mpya.
Akamwambia: Ifute, akaifuta.
Kisha baba akamuuliza kijana wake: Je karatasi bado ni nyeupe (ina sehemu ya kuandikia)?
Kijana akajibu: ndio, Lakini baba umekusudia nini???
Baba akamshika kijana wake begani, akamwambia: Kijana wangu, ndoa yahitaji ufutio.
Iwapo kama huto kuwa na ufutio katiaka ndoa yako, ili uweze futa baadhi ya mambo au matukio ambayo hufurahishwi nayo kutoka kwa mkeo, na mkeo vile vile ikiwa hato kuwa na ufutio ambao anaweza futia baadhi ya mambo na matukio ambayo hafurahishwi nayo toka kwako, basi ukurasa wa ndoa utajaa maandishi kwa masiku machache sana!
Ujumbe huo wa leo umekuja kwa msaada wa MIMI MUISLAM ndani ya FACEBOOK.
0 comments