JUMLA ya wachezaji 20 wa mchezo wa kuogelea wamepatikana katika mashindano ya mchujo wa kutafuta timu itakayoshiriki michuano ya Afrika Mashariki inayotarajiwa kufanyika Oktoba 22-23 Kampala, Uganda.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Chama cha Kuogelea, Marcelino Ngalioma, alisema kuwa wachezaji hao wamepatikana baada ya kumalizika kwa mashindano maalumu ya kuwasaka yaliyofanyika katika awamu sita.
Aliwataja waogeleaji hao kuwa ni pamoja na Sonia Tumiotto, Talin Stengel, Marcel Awori, Rishi Somaiya, Nella Marais, Angenie Tayler, Agnes Kimimba, Shamrad Magesveran, Erick Mlima, Danielle Awori, Iyas Shivji, Patrick Kimimba na Shreyashi Chowdhury.
Wengine ni Godfrey Masishanga, Philipo Sagareti, Omari Abdallah, Ali Bamba kutoka Zanzibar, Hilal Hilal, Adam Kitululu na Nduruma Majembe.
Ngalioma alisema kuwa kamati ya ufundi imemteua Ramadhani Namkoveka kuwa kocha mkuu wa timu hiyo ambayo inatarajia kuingia kambini Oktoba 16 kujiandaa na mashindano hayo.
Tanzania daima
0 comments