Friday, November 11, 2011

Mbeya si shwari

TAARIFA ILIYOIFIKIA GLOBU YA JAMII HIVI PUNDE KUTOKA JIJINI MBEYA,INAELEZA KWAMBA KUMEZUKA VURUGU KUBWA SANA JIJINI HUMO KATI YA WAFANYA BIASHARA NDOGO NDOGO AMBAO WANAPANGA BIDHAA ZAO NJE YA SOKO LA MWANJELWA NA ASKARI WA JESHI LA POLISI.

VURUGU HIZO ZIMEZUKA MARA BAADA YA WAFANYA BIASHARA HAO KUANZA KUWAPIGA KWA MAWE MGAMBO WA JIJI WALIOKUWA WAMEFIKA SOKONI HAPO ILI KUWAONDOA WAFANYA BIASHARA HAO KUFUATIA KAULI YA MKUU WA MKOA WA MBEYA,MH. ABBAS KANDORO YA KUWAONDOA WAFANYABIASHARA WOTE AMBAO WALIKUWA WAMEPANGA BIDHAA ZAO BILA MPANGILIO,KIASI KWAMBA HATA BARABARA YA KUPITA MAGARI INAKUWA IMEFUNGWA KUTOKANA NA BIASHARA ZAO.

ASKARI WA JESHI LA POLISI WAMEFIKA KATIKA ENEO HILO MUDA HUU NA KUANZA KUTULIZA GHASIA HIZO HUKU NA WAO WAKIENDELEA KUPIGWA MAWE NA WAFANYA BIASHARA HAO, HALI ILIYOWALAZIMU KUTUMIA MABOMU YA MACHOZI KUTULIZA GHASIA HIZO.

KUTOKANA NA GHASIA HIZO, HALI IMEKUWA TETE KWA WAKAZI WA MAENEO YA JIRANI NA ENEO HILO LA SOKO NA KUSABABISHA WATU WENGINE KUKIMBIA MAKAZI YAO KWANI WAFANYA BIASHARA HAO WAMEKUWA WAKIANGUSHA MVUA YA MAWE KWA ASKARI HAO,HUKU WAFANYA BIASHARA HAO WAKIWA WAMEANZA KUCHOMA MOTO MATAIRI NA KUPANGA MAWE BARABARANI.

Michuzi


Kwa taarifa zilizoendelea kusambaa kwenye mhtandao na vyombo vya habari toka Mbeya, vinasema mabomu ya machozi yame mininika.

0 comments