Monday, December 26, 2011

JE INAFAA KWA MUISLAMU?

Assalam Alaykum warahmatullah wabarakatuh.

Katika pita pita katika mitandao nimejikuta nikitua katika ukuta wa Facebook wa Habiba Abdul Malemba ambapo kulikuwa na ujumbe ulio wekwa na Salim Juma Salim ambao unaenda kwa anuwani ya "JE INAFAA KWA MUISLAMU?"

TUKAPATE JAWABU

Usikubali kushindwa, shetani akakuteka,
Utageuka mfungwa, wa shetani ni mateka,
Hapo umeshaangushwa, na imani kutoweka,
Mtihani Ukifika, Subira Inatakiwa.
Hapa nafunga baruwa, pengine mmeshachoka,

Tunaomba maridhawa, Mola Apate Ridhika,
Tunaomba kuepushwa, na madhambi kufutika,
Mtihani Ukifika, Subira Inatakiwa.

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Kula chakula cha Mkristo haikatazwi na Dini ya Kiislamu bali zimekuja nasw za moja kwa moja kuhusu jambo hili.

Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema: “Na chakula cha wale waliopewa kitabu ni halali kwenu na chakula chenu ni halali kwao” (5:5).

Na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwapa ruhusa ya kufanya hivyo.

Kwa hivyo ki-msingi kula chakula chao kinaruhusiwa kwa Muislamu ila kiwe tu ni cha halali. Ikiwa ni chakula ambacho ni haramu kwetu basi itakuwa haifai kula chakula hicho au kikiwa kimechanganywa chakula ambacho ni haramu na kile kilicho halali, hivyo kukifanya chote kuwa haramu.
Lakini unapozungumzia kuhusu sherehe zao ambapo kutakuwa na chakula kwa kuadhimisha siku kuu hiyo yao inakuwa haifai kwa Muislamu kushirikiana nao katika jambo hilo.

Hivyo, ukialikwa na Mkristo kula nao chakula cha Krismasi inafaa ukatae kwani si halali kabisa, lakini ikiwa ni siku ambayo si sherehe kwao unaweza kula bila ya matatizo yoyote.

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipohamia Madiynah, watu wa Madiynah walikuwa na siku kuu zao ambazo walikuwa wanasherehekea, naye (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akawaambia kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Amewabadilishia kwa siku ambazo ni bora zaidi, nazo ni: 'Iyd baada ya Ramadhaan na 'Iyd ya baada ya Hijjah.

Hivyo, haifai kwa Muislamu kusherehekea siku kuu nyengine zozote mbali na hizo hata zile ambazo Waislamu wenyewe wamezizua kama za Mawlid na mwaka mpya wa Kiislamu na zingine kama za Mi'iraaj na Niswf Sha'abaan.

Na Allaah Anajua zaidi

0 comments