Monday, February 13, 2012

One year on Blogger


Ilikuwa ni February 21 ambapo Abdallah Hamdun Ibrahim Sulayman (Aboodmsuni) alijisajili katika blogger, na kuitambulisha/kuanzisha Aboodmsuni Na Soka La Bongo wakati huo ikijulikana kama Tanzania Football Event, wiki tatu baadae atatmbulisha blog ya Aboodmsuni Home wakati huo ikitambulika kama Tafakari Na Bonge.

Wakati anaanza na Aboodmsuni Na Soka La Bongo alikuwa nchini Sudan akisoma lugha ya kiarabu ambapo alitoka nchini humo mwezi wa tano, na kurejea Tanzania huku akiendelea kuendesha blog zake mbili za Aboodmsuni Na Soka La Bongo na Aboodmsuni Home kabla ya mwezi wa sita mwaka jana kupewa jukumu la kuenbesha blog ya mashabiki wa Azam FC katika Azam Fans Club.

MAFANIKIO

Mafanikio yaliyopatikana katika mwaka huu wa kwanza katika tasnia ya blogger ni kushika katika nafasi nne za juu katika Tanzania Best Sports Blog 2011 na katika Best Informative Sports Blog 2011.
Aboodmsuni Na Soka La Bongo ilikuwa Second runner katika Tanzania Best Sports Blog 2011 na Aboodmsuni Home ilikuwa Third runner katika Best Informative Sports Blog 2011.

Aboodmsuni Na Soka La Bongo imekuwa ikiongeza idadi ya watu wanaotembelea siku hadi siku na kwa sasa wanatembelea watu 300-700 kwa siku, wakati Aboodmsuni Home ikiwa na idadi ndogo ya watu wanaotembelea ambapo 30-100 kwa siku.

SHUKRANI

Mafanikio niliyo yapata katika mwaka wa kwanza katika tasnia ya blogger kwa kiasi kikubwa kimechangiwa na group la Kandanda, Sports xtra clouds fmndani ya Facebook ambapo kwa kiasi kikubwa nilikuwa napata update za michezo ambayo sikupata wasaa wa kufika kiwanjani. Natoa shukrani kwa member wote wa group hizo mbili.

Pia natoa shukrani kwa kurasa za Azam FC, Young Africans Sports Club na Coastal Union za facebook. Kurasa zote hizo zinarahisisha shughuli mbalimbali za Aboodmsuni Na Soka La Bongo.

Na hitimisha kwa kutoa shukrani kwa dada wa Aboodmsuni, Khadija, Jannat na mdogo wake Osama kwa sapoti walionipatia bila kumsahau Patrick Kahemele na blogger Shaffih Dauda wa Shaffih Blog Sport na Dina Ismail wa Dina Ismail

0 comments