Monday, February 27, 2012

'Wataalam wapo hawatumiki' tofauti za kisiasa

Kwenye pita pita katika mitandao ya jamii hii leo nikajikuta natua katika status ya Semeni Nyerere inayosema kuwa;


Prof Ibrahimu Haruna Lipumba, anatarajiwa kutua nchini kutoka Ulaya ambako Majuzi alichaguliwa kuwa MWENYEKITI/RAIS WA MAPROFESA WOOOOTE WA UCHUMI DUNIANI Baada ya kuwabwaga na kuwashinda kwa kura nyingi zaidi ya Maprofesa 555 kutoka sehemu mbalimbali za Duniani.

Yatakuwa ni mapokez makubwa ambayo hajawah tokea, Pia Rais Wetu mpendwa JK amevunja ukimya amesema atakuwepo kumlaki, Kagame wa Rwanda amempongeza Sana Prof LIPUMBA kwa kumfananisha na Mshambuliaji machachari wa Barcelona ya zamani SAMUEL ETOO, na amesema ni swala la kujivunia kuwa mtaalamu wetu kutoka Africa wametambua mchango na umuhimu wake.

Mimi shida yangu ni kwamba KAMA MPAKA WATAALAMU NA MAPROFESA WA UCHUMI WA MATAIFA YALOENDELEA WAMEMKUBALI lipumba na kumpa hadhi kubwa namna iyo mbona sisi hatumtumii? Tunamuona kama Mbwa tu?

Haya mambo ya vyama vya siasa yasiwe vgezo vya kuteua watenda kazi wa SERIKALI, kama MTU ni Mtaalamu Serikali impe cheo kikubwa atumikie taifa bila kujali anatoka chama gani.

Mfano Lipumba angepewa hata UWAZIRI WA FEDHA MAANA MKULO KASHNDWA hata UGAVANA WA BENKI KUU mana hata BENO NDULU hakuna anachokifanya Shauri yetu wataalamu 2nao 2mewasomeshwa kwa hela ya serikal na kod za wananchi ila hatutaki kuwatumia badala yake 2nazngatia U-ccm, U-cuf, U- chadema halafu ugumu wa maisha unatupga kama kawa.

Nahs TUMELOGWA Obama pamoja na kwamba ni Democtract lakini katka uongoz wake kagawa nafas nying kubwa kubwa wapinzani akiwemo WAZIRI WA ULINZ Ambaye ni REPUBLICAN, nahs kwa watanzania hyo ndoto, Ukiwa chama pinzani wewe NGEDERE tu hutakaa uckilzwe hata kama ni MTAALAMU KIASI gani, ila ukiwa chama tawala hata Kama wewe MBUMBUMBU mawazo yako yataskilzwa na kufanyiwa kazi.


SAFARI NI NDEFU. CONGLATURATIONS PROF. HARUNA LIPUMBA GOD BLESS U!


Mwisho wa nukuu waweza bofya hapa kuona maoni ya wadau wa Semeni

0 comments