Blogger Abdallah Hamdun Sulayman 'Aboodmsuni' wa Sports In Bongo (SIB) anataraji kuanza mtihani yake ya kumaliza mwaka April 23, kitendo kitakacho punguza ufanisi wa utoaji habari katika Sports In Bongo katika mwezi huo.
Kutokana na kalenda ya mitihani ya kufunga mwaka kukaribia pamoja na harakati ya kutafuta mahali pakufanyia Industrial Training (field) mara baada ya kumaliza mitihani ya mwaka, kutapelekea kuchelewa na kupunguwa kwa taarifa mbalimbali za kimchezo ndani ya Sports In Bongo ambayo inasimamiwa na Aboodmsuni.
Twawaomba samahani kwa wasomaji wetu wa Sports In Bongo na wafuatiliaji wa mitandao ya Aboodmsuni kwa usumbufu ulioanza na kuendelea kujitokeza katika kipindi chote cha mwezi April.
Ni matarajio yetu kurejea katika kasi yetu mara baada ya kumaliza mitihani hiyo ya kufunga mwaka.
No comments:
Post a Comment