Na Nova Kambota,
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Wilaya ya Mkuranga kimezidi kujiongezea umaarufu wake kwa kuzidi kusomba wasomi wengi wilayani humo. Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Mkuranga Bw Jamal Lwei amekaririwa akisema...kwetu haya ni mafanikio makubwa kwani chama sasa kinakua kwa kasi na wasomi wanaonekana kukubali mipango, sera na harakati zetu....
Mwenyekiti huyo aliyasema hayo mapema leo asubuhi huku pia akitoa salamu za pole kwa baadhi ya wanamkuranga waliofikwa na maafa kutokana na mvua zilizoambatana na upepo siku ya jana , ambapo taarifa za awali zinabainishwa kuezuliwa kwa mapaa ya baadhi ya nyumba za wananchi wa wilaya hiyo na nyingine kuangukiwa na miti.
Mwenyekiti huyo pamoja na mambo mengine pia amezungumzia uchaguzi wa Arumeru Mashariki huku akisisitiza kuwa ana imani wana Arumeru watamchagua Nassari kutokana na uwezo wake mkubwa wa kusimamia sera za kimaendeleo.
Duru za kisiasa kutoka jimbo la Mkuranga ambalo linashikiliwa na Adam Malima zinabainisha kuwa sababu ya wasomi wengi kuhamia CHADEMA ni pamoja na kushindwa kwa sera za CCM za maisha bora kwa kila mtanzania huku wananchi wakiendelea kusota kwenye umasikini mkubwa huku viongozi wa serikali hasa wale wateule wa rais Kikwete wakiogelea kwenye utajiri mkubwa. Baadhi ya wananchi wameenda mbali zaidi huku wakihoji kuhusu mgao wa umeme, matokeo mabovu ya shule za sekondari na msingi pamoja na huku wakiishinikiza serikali iwalipe malipo ya fedha za korosho ambazo wamesema bado hawajalipwa.
No comments:
Post a Comment