Monday, May 7, 2012
Msuni atinga Mikovilla usiku mnene
Mmiliki wa Aboodmsuni Network, Abdallah Hamdun Ibrahim Sulayman 'Aboodmsuni' ama Msuni kama watu wa Mikovilla wanavyo muita alirejea kitaani Mikovilla jana Usiku akitokea Morogoro.
Msuni alianza safari ya kurejea Mikovilla mtaa ambao unapatikana Mikocheni B jijini Dar es salaam mchana wa jana lakini kwa mara ya kwanza alirejea Mikovilla usiku wa saa 5, ambapo hakuwahi kutoka ama kurejea Mikovilla zaidi ya saa 3 usiku, lakini jana alifanya hivyo kwa mara ya kwanza.
Msuni alitua Ubungo saa 12 jioni na kuelekea moja kwa moja Posta Mpya, ambapo alialikwa na Azam FC katika tafrija ya kufunga msimu wa 2011/12, ambapo walitwaa nafasi ya pili.
Taarifa ya kilicho jiri katika tafrija hiyo itakuwa ndani ya Sports In Bongo 'SIB', na Msuni alitoka katika ukumbi saa 4 usiku ikiwa ni mara yake ya kwanza kuwa posta mda huo, na kupata lifti mpaka Magomeni na ndipo alipochukua usafiri wa kurejea maskani kwake Mikovilla.
Msuni anapenda kuwa taarifu Aboodmsuni Network imerejea baada ya kumaliza likizo yake fupi mkoani Morogoro, vile vile anapenda kuwapongeza Simba SC kwa kutwaa Ubingwa na kumpatia misumali 5 mpinzani wake wa jadi Yanga.
No comments:
Post a Comment