Friday, June 15, 2012

SIB yateuliwa katika kinyanganyiro cha Best Sports Blog

 Aboodmsuni Network mwaka huu imefanikisha kuingiza blog moja katika mashindano ya Tanzania Best Blog baada ya mwaka jana kuingiza blog mbili katika vipengele viwili tofauti na kufany vyema katika vipengele hivyo.

Blog ya Sports In Bongo ambapo hapo awali ilikuwa inafahamika kwa jina la Tanzania Football Event mwaka jana iliambulia kuwa third runner katika kipengele cha Best Sports Blog wakati Aboodmsuni Network iliyokuwa inatmbulika kwa jina la Aboodmsuni Home ilifanikiwa kuwa second runner katika kipengele cha Best Informative Sport Blog ambcho mwaka huu hakipo.

Mwaka huu wa 2012 kati ya blog tatu zinazo simamiwa na Aboodmsuni Network ni blog moja ndio iliyopendekezwa na wadau kushiriki kwenye kinyanganyiro cha kusaka Best Blog in Tanzania ambayo ni Sports In  Bongo iliyoingizwa kwenye kipengele cha Best Sports Blog kwa mara nyingine tena.

Twatoa shukurani kwa wadau wetu waliitupendekeza kushiriki na wasimamizi wa shindano hilo ambao ni Tanzania Blog Awards kuipitisha na kuwaachia wadu kupiga kura, ambapo kura zitaanza kupigwa juni 17 mpaka mwishoni mwa mwezi huu katika website yao (www.tanzanianblogawards.com)
 .

Blog nyingine zilizopo katika kipengele hicho ni pamoja na:
http://aboodmsuni.blogspot.com

No comments:

Post a Comment