Na Fatma Aboud Athman, Facebook. Nizikani ni ngali hai, nifapo munisitiri. Sifanyi sitihzai, sitaki utiriri, kama kweli mwanidai, musinifanyie ni siri, nenani ni ngali hai, wakati haujajiri. Siku hiyo nikinyoka, denilo sitasema, nitakua nimewatoka, sitokua nayo kalima, hakiyo utaitaka, kuepukana na lawama, mimi siifanyi dhihaka, mdai hebu leo simama. Na kama wanijali, siningoje moyo kutuwama, ukaupika wali, ulotanganywa ni nyama, nipa nile nijenge mwili, niwe na afiya njema, singoje kifo adiili, uwape wana kwa watu wazima, kama wataka kunisifu ruhusa mekupa sasa, usingoje mekuwa mfu, upitapo masikini mayasa, aliko ni maarufu, kwa kuyaa na kupusa, urongo sitaki uusadifu, Mola motoni takupisa. Tamati nimeyasema, kifo ni dhia ya haki, nami sichi kulitema, madamu sijafariki, narudi kuketi nyuma, niwasikize marafiki, munizike ningali mzima, munisitiri nikifariki.
Thursday, October 4, 2012
KUTOKA FB: KIFO DHIHAKI

0 comments