Monday, January 28, 2013

VPL ROUND UP: TEGETE GOLI 5 KATIKA MICHEZO MITATU 3

Ligi kuu ya vodacom (vpl) iliendelea mwishoni mwajuma lililopita ikiwa ni mchezo ya awali ya mzunguko wa pili wa ligi hiyo. Yafuatayo ni matukio yaliyojiri katika michezo hiyo 7 iliyochezwa katika viwanja sita yakiweka katika mtindo wa namba;

0. HAKUNA SARE

Katika michezo iliyocheza mwishoni mwajuma lililopita hakukushuhudia sare ya aina yoyote ile zaida ya matokeo ya ushindi na kufungwa katika michezo yote 7 ya ligi kuu ya vodacom


1. POLISI MORO WAPATA USHINDI WA KWANZA

Polisi Morogoro jumamosi walipata ushindi wao wa kwanza toka ligi kuu ya vodacom 2012/13 ianze pale walipo wafunga Mtibwa sugar goli 1-0 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Manungu.

MCHEZO MMOJA ULIOSHUHUDIA MWENYEJI AKIFUNGWA

Mchezo baina ya Mtibwa sugar na Polisi moro ndio mchezo pekee ulioshuhudia mwenyeji akilala kwa goli 1-0 huku michezo mingine 6 wakishuhudia wenyeji wakitoka na ushindi. Katika mchezo huo Mtibwa sugar alikuwa mwenyeji.


2. REDONDO AFUNGUWA UKURASA WA MABAO KATIKA DURU LA PILI

Kiungo wa simba sc Ramadhani Chombo (Redondo) alikuwa wa mwanzo kuzinna nyavu katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya vodacnm msimu huu baada ya kuifungia simba sc goli katika ushindi walioupata wa goli 3-1 mbele ya African lyon akiwa amefunga katika dakika ya 2 ya mchezo.

PENATI MBILI ZA KOSWA KATIKA MCHEZO MMOJA.

Katika mchezo kati ya simba na african lyon kulishuhudia penati mbili zikikoswa. Walianza lyon kupata penati iliyopigwa na Ally Shamte aliyekosa na simba wakakosa penati yao iliyopigwa na Mrisho Ngassa.


3. MECHI TATU KATIKA ARDHI YA TANZANIA GOLI 5.

Mshambuliaji wa yanga Jerryson Tegete ameonyesha uwamba wake wa kucheka na nyavu baada ya kufikisha goli 5 katika michezo mitatu toka mwaka uwanze aliyocheza akiwa na yanga hapa nchini Tanzania.

Tegete amefunga goli 5 katika michezo mitatu mfululizo akianza na goli 2 katika mchezo wa kwanza dhidi ya black leopards na kufunga goli 1 katika mchezo wa marejeano na kukamilisha goli 2 katika ushindi wa goli 3-1 dhidi ya prisons.


5. MICHEZO MITANO YA MALIZIKA KWA USHINDI WA GOLI 3-1.

Michezo tano kati ya saba ya ligi kuu ya vodacom ilishuhudia matokeo ya ushindi wa goli 3-1, michezo hiyo ni:
SIMBA 3-1 AFRICAN LYON
AZAM 3-1 KAGERA SUGAR
YANGA 3-1 PRISONS
COAST UNION 3-1 MGAMBO
OLJORO JKT 3-1 TOTO


--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA COMPUTER YAKO
call us: +255-657-184-421
www.aboodmsuni21.blogspot.com

No comments:

Post a Comment