Thursday, February 21, 2013

ABOODMSUNI NETWORK YATIMIZA MIAKA MIWILI

Wamiliki wa blog ya SPORTS IN BONGO na wasimamizi wa blog ya AZAM FANS CLUB, ABOODMSUNI NETWORK mchana wa leo wanataraji kutimiza miaka miwili toka waanze kutoa huduma rasmi.

Abdallah Hamdun Ibrahim Sulayman (Abood ama Msuni) alipata wazo la kuanzisha ABOODMSUNI NETWORK (AN) baada ya kufanya kazi yautowaji msaada kwa watu wanaotatizika kutumia computer na mtandao wa internet kwa takriban miezi saba ikiwa sambamba na utoaji wa matokeo ya michezo mbalimbali ya ligi kuu ya Tanzania kwa rafiki zake wakiopo nnje ya nchi wakati Msuni bado ajaenda Sudan oktobar 20 mwaka 2010.

Kutokana na rafiki zake kuendelea kuhitaji matokeo wakati Msuni hayupo nchini kuliibua fikra ya kuja na ABOODMSUNI NETWORK mchana wa jumatatu february 21 mwaka 2011 na ktjiwekea malengo ambalo lengo kuu katika mwaka wa kwanza ni kusimamisha blog ya matukio ya mpira wa miguu yanayojiri nchini Tanzania.

Mida ya saa moja kasoro usiku akitokea kwenye darasa la kusoma kiarabu akiwa katika jiji la Khartoum Sudan ndipo TANZANIA FOOTBALL EVENT (sasa inafahamika kama SPORTS IN BONGO).

ABOODMSUNI NETWORK ilifungua blog nyingine ya TAFAKARI NA BONGE (sasa inajulikana kama ABOODMSUNI NETWORK) ikiwa na malengo ya kuzungumzia mikakati ya Msuni, shughuli za AN pamoja na fikra mbalimbali za Msuni na wadau wake ikiwa ni wiki mbili toka SPORTS IN BONGO ianze kazi.

AN ilizindua rasmi huduma ya kukarabati (computer repair) mwishoni mwa mwaka 2011, hapo awali ilikuwa inatoa msaada katika utumiaji wa computer.

Tunatimiz miaka miwili tukiwa na watembdleaji katika blog ya SPORT IN BONG (Blog viewer) 1000-3000 kwa siku vile vile tukipata cheti toka kwa AZAM FC katika kuikubali kazi tunayo ifanya.

Pamoja na kukubwa na ukata katikati nusu ya pili ya mwaka wa pili katika kuelekea kutimiza mwa wapili huku vitendea kazi vikipotea na kuharibika katika mazingira ya kutatanisha tunawaomba radhi wadau wetu kwa usumbufu uliojitokeza.

Tunapenda kutoa shukurani kwa mtangazaji wa COCONUT FM ya Zanzibar Ally Mohamed kwa msaada alio utoa kwa SIB, bila kuwasahau ma admin wa kurasa ya yanga, azam na coastal union ndani ya facebook na wadau wanao patikana katika makundi ya kandanda, sports xtra na ligi kuu Tanzania ndani ya facebook.

Tumefika hapa tulipo kwa msaada wa wadau na wateja wetu, wote tunawashukuru kwa kuiunga mkono na kuendelea kuikubali ABOODMSUNI NETWORK


--
MSUNI COMPUTER SOLUTION TUPO PEMBA FEB 21-MACH 15
TUNAREKEBISHA COMPUTER ZILIZO KUFA
Wasiliana na HABIB KHAMIS: +255-657-148-283
www.aboodmsuni21.blogspot.com

0 comments