Mchezo huo utakao chezwa siku ya jumatano kuanzia mishale ya saa 10 alasiri na michezo mingine itakayo chezwa siku hiyo haitakuwa na matokeo yake katika ukurasa wa dakika 90.
Hali hiyo inasababishwa na muendeshaji wa kurasa hiyo bwana Abdallah Sulayman 'Abood' kuwa katika kipindi cha mitihani ya kumaliza semister ambayo inataraji kuanza hapo kesho jumatatu (february 11) na kuhitimishwa ijumaa (february 15).
Kuingia katika kipindi cha mtihani kwa Abood kutaathiri pia baadhi ya shughuli za ABOODMSUNH BLOGS ambazo zinataraji kutimiza miaka miwili toka ianzishwe february 21 mwaka 2011.
Tunaomba mtuwie radhi kwa usumbufu utakao jitokeza na ni matumaini yetu ukurasa wa dakika 90 kurejea katika shughuli zake hapo jumamosi ya february 16 katika mchezo kati ya azam na al nasri ya Sudan.
--
Abdalah Hamdun Ibrahim Sulayman
C.O ABOODMSUNI NETWORK
+255 657 184 421
aboodmsuni@yahoo.com
No comments:
Post a Comment