Jana nilifahamishwa na rafiki yangu mmoja kwamba ametumiwa barua pepe
inayoonyesha kutoka kwa mwanasiasa mmoja wa huko Tanzania. Katika e-mail
hiyo, mwanasiasa huyo anaonekana kulalamika kuhusu post 'iliyowekwa' na
rafiki yangu huyo japo hakuna post aliyoweka.
Sasa jinsi gani matapeli hao wanavyojaribu kuku-trick uwapatie password
yako? Wanakupa link wanayodai ndio yenye post yako huko Facebook, lakini
ukiibonyeza inakutaka u-log into akaunti yako ya Facebook. Kimsingi
link hiyo sio ya Facebook bali inalenga kunasa password yako.
Mara nyingi hackers (wezi wa password) wanacheza sana na hisia za
mlengwa wao. Kwa mfano katika mbinu hii wanafahamu kuwa pindi ukipata
e-mail inayokulaumu kwa kosa mbalo hujalifanya unaweza kukurupuka kwa
hasira kutaka kumthibitishia huyo anayekutuhumu kwamba hujafanya kitu
kama hicho.
Tahadhari muhimu kuhusu hackers ni kwamba pindi upatapo e-mail za
'kisanii' kama hiyo aliyotumiwa rafiki yangu, IFUTE HARAKA SANA.
Usihangaike kuwajibu kwa sababu unapo-reply e-mail kuna information
flani kwenye "full header" inayoweza kumpatia hacker taarifa za
kukuhujumu.
Basi tafadhali mfahamishe na mwenzako kuhusu utapeli huu mpya.
As always, SHARING IS CARING
0 comments