Wednesday, February 18, 2015

MAMILIONI YA DOLA YAIBIWA KATIKA MABENKI KUPITIA WIZI MTANDAO



Baada ya kikao kilichofanyika wiki iliyopita chuo kikuu cha Stafford ambapo Rais Obama wa marekani alikutana na wafanya biashara, Wanasheria na wasimamizi washeria kujadili hali ya mtikisiko wa maswala ya usalama mitandao, Inadhihirisha wazi bado kuna safari ndefu kukabiliana na wimbi hili la uhalifu mtandao duniani kote.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba Tishio la uhalifu mtandao na utayari wa kukabiliana nao bado kuna kutowiana ipasavyo ingawa jitihada bado ni kubwa kuweza kukabiliana na uhalifu huu unaokua kwa kasi ya pekee duniani kote.

Nategemewa kuwasilisha mada itakayoangazia jitihada za mataifa makubwa 8 dhidi ya uhalifu mtandao na athari za jitihada hizo kwa mataifa mengine katika mkutano wa mwaka utakaofanyika Nchini Croatia unaounganisha wataalam wa maswala ya usalama mitandao kutoka mataifa kadhaa ambapo patajadiliwa mambo kadhaa ya kiusalama mitandao – Taarifa Zaidi za mkutano zinaweza kupatikana kwa "KUBOFYA HAPA"

Wakati haya yakijiri na mikakati Zaidi ikiendelea ya kukabiliana na wimbi kubwa la uhalifu mtandao hivi sasa makampuni yanayojihusisha maswala ya fedha yameonekana yakiathirika Zaidi na uhalifu mtandao – Hii ni kwamujibu ya ripoti maalum iliyotolewa na kampuni ya Kaspersky Lab. ZAIDI BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment