Sunday, February 21, 2016

TUMETIMIZA MIAKA 5, SHUKRANI KWAKO MDAU WA SPORTS IN BONGO

Jumatatu februari 21 mwaka 2011 mida saa moja usiku ndipo blog ya Sport In Bongo ilipofunguliwa ikienda na jina la Tanzania Football Event na post yake ya kwanza iliwekwa jumanne ya fevruari 22 mwka huo ikiwa na kichwa cha habari Majimaji ya timuwa kocha.

Toka blog hiyo ya sports in bongo ianze hii leo inatimiza miaka mitano, ambayo inamfanya Mmiliki na mtendaji pekee wa Aboodmsuni Network Mr. Abdallah H.I Sulayman naye kutimiza miaka mitano toka aanze shughuli za blog.

Sport In Bongo ndio ilikuwa blog yake ya kwanza, ambayo aliitengeneza mwenyewe na bado anaifanyia maboresho mwenyewe, kabla ya kuhusishwa katika utengenezaji wa blog kadhaa ambazo zingine zimeshindwa kuendelea na zingine bado ziko hewani.

Kwa sasa Abdallah H.I Sulayman (Msuni) anasimamimia blog zake 4 ambazo ni Chama Langu Azam FC, Tembezi Za Msuni, Aboodmsuni Network na Sports In Bongo inayotimiza miaka mitano sasa.

Msuni anapenda kutoa shukurani zake kwa wadau wote waliofanikisha blog ya Sport In bongo kuendelea kuwepo na kufanya kufikisha miaka mitano hii leo.

Ni ahadi yetu kuendelea kutoa update katika blog zetu, na kuendelea kukiboresha kipengele pendwa katika blog ya Sport In Bongo kipengele cha SIB Dakika 90 kinachomuwezesha mdau kupata matokeo ya moja kwa moja, msimamo wa ligi, sambamba na orodha ya wafumania nyavu.

Shukrani za dhati kwa waendeshaji na wasimamizi za website ya Mbeya City, Azam FC na TFF, wamiliki na wasimamizi wa blog na webzite za Salehjembe, Bin Zubeiry, Shaffih Dauda online, Boi Plus, Habari Leo, na nyinginezo ambazo kwa hali moja ama nyingine imetuwezesha kufikia hapa tulipo.

Vile vile twamshukuru Ally Mohammed wa coconut FM, Patrick Kahemele, Dismas Ten, Dina Ismail na wengineo kwa ushirikiano waliotoa na kuendelea kuutoa kwetu.

Twahitimisha shukran zetu kwako msomaji na mfuatiliaji wa blog zetu kwa sapoti unayotuonyesha kwetu, kwani dhumuni ya kuweka taarifa ni ili isomwe na wasomaji ni nyinyi.

Imetolewa Na Abdallah H.I Sulayamn
Mmiliki wa Aboodmsuni Network

No comments:

Post a Comment