Saturday, August 13, 2016

APP SIB 90 IPO TEYARI KWAKO MDAU WA SIB DAKIKA 90

Wakati ligi kuu ya Tanzania Bara ikibakisha wiki moja kuanza kwa msimu wake mpya. Aboodmsuni Network kwa kutambua kuwa wasomeja wengi wa Blog zao ni wapenzi wa ligi hiyo, imeendeleza utamaduni wake wa kuboresha kipengele chake cha SIB Dakika 90 kinachopatikana ndani ya blog ya Sports In Bongo.

Maboresho ya mwaka huu ni ya kumuwezesha mfuatiliaji wa soka la bongo kuendelea kupata matokeo ya mechi mbalimbali kupitia simu yake katika bidhaa mpya ya Aboodmsuni Network inayo kwenda kwa jina la SIB-90.

SIB-90 ni application ya simu ambayo itamuwezesha mtumiaji kupata mambo yote yaliyokuwa yanaendelea katika kipengele cha SIB Dakika 90 kilichopo katika blog ya Sports In Bongo.

Application ya SIB 90 itakuwezesha kufutailia michezo matokeo ya mechi zinazo husisha timu za Tanzania moja kwa moja (livescore) kuangalia mtokeo ya mechi zilizopita, ratiba, msimamo wa ligi kuu ya vodacom na msimamo wa wafungaji bora.

SIB 90 kwa sasa haitopatikana katika google play store badala yake inapatikana katika  APTOIDE.

Na vile vile inapatika katika google drive kupitia link hii: https://drive.google.com/file/d/0B-TC45mUrSckeVgwRUZlbVM3N1k/view 

Uwepo wa SIB 90 si kigezo cha usitishwaji wa kipengele cha SIB Dakika 90, bali vyote vitaendelea kufanya kazi kwa pamoja.

Imetolewa na Abdallah H.I Sulayman
Mmiliki na mtendaji wa Aboodmsuni Network

sadsdfdsffdff

No comments:

Post a Comment