Sunday, October 15, 2017

MSUNI AIWAKILISHA VYEMA ABOODMSUNI NETWORK NCHINI UGANDA

Timu ya mafundi katika kliniki ya computer iliyofanyika jana katika chuo cha kiislamu Uganda, kampusi ya Mbale
Mmiliki na mtendaji mkuu wa AboodmsuniNetwork Abdallah H.I Sulayman (Abood Msuni) alijumuika na team yake ya Halaba katika zoezi la urekebishaji wa komputer na kutoa mafunzo ya namna ya kutumia na kutunza komputer iliyokuwa imeandaliwa na serikali ya wanafunzi ya chuo kikuu cha kiisalam Uganda kupitia waziri wake wa ICT Mr. Ally Othman Ally.

Zoezi hilo lilifanyika kkatika kampus kuu ya chuo hicho iliyopo Mbale, Uganda ambapo Abood Msuni alishungulika zaidi katika upande wa software na kutoa maelekezo ya namna ya kutumia computer bila kupata matatizo yoyote.
Habib Ally Khamisi (Halaba Member na RAHASO member) akiwa anarekebisha moja ya computer iliyofika mezani mwake
Shughuli hiyo iliyoanza saa nne asubuhi na kuhitimishwa saa kumi na mbili jioni iliwahudumia wanafunzi na baadhi ya wafanyakazi wa chuoni hapo, ambao walikuwa na matatizo ya computer zao.




No comments:

Post a Comment