Thursday, June 2, 2011

Imani ya dini yaleta mtafaruku katika mazishi

Siku ya jumatatu katika mkoa wa Iringa katika enelo linaloitwa Kihesa Mwangingo ambako kijana alikufa kwa ukosefu wa damu na katika mazishi yake, kulitawala kila aina ya mmbeleko.

TOKA IRINGA MJINI, SOPHIA SALEH ANATUJUZA KILICHOTOKEA.
Mzee huyo ajulikanae kwa jina la mzee Sigara ambae ni muumini wa mashahid wa yehova. Alikuwa anauguliwa na kijana wake wa kiume na tatizo la kisayansi lilipofanywa na madaktari ikagundulika kuwa kijana huyo ana upungufu wa damu, ndipo madaktari wakashauri kijana huyo aongezewe damu. Kutokana na imani kali ya muumin huyo alikataa kijana wake asiongezewe damu kwa kusisitiza kuwa dini yake hairuhusu na ni dhambi kubwa kumuongezea mtu damu. Hatimaye madaktari wakaamua kumuacha na msimamo wake huo kama mzazi licha ya kupata ushauri mbalimbali.

Siku ya tukio kijana yule alifariki na taratibu zote za mashahd ya yehova zilifuatwa ikiwemo kutokuimba mapambio wala nyimbo za maombolezo, kutokuaga mwili wa marehemu na mwili ulifikishwa makaburini kwa ushirikiano wa vjana wa mtaani kushughulikia kuchimba kaburi kama ilivyokawaida ya maswala haya kwenye jamii zetu.
Kasheshe ilianza mara baada ya mwili ulipofikishwa makaburini, hapo ndio kundi kubwa la vjana lilifika likiwa mna bakora a.k.a fimbo mikononi kiasi cha nusu tani ya lundo la fimbo na kukusanywa sehemu moja.

Mpango mzima huko makaburini ulikuwa kama move na hii ni zaidi ya zile filamu zetu za kiafrika kama za kina Kanumba na za kina Noa Ramsei maana hii ilikuwa imebamba mbaya.Vijana walikuwa wamejiandaa vya kutosha, kwa ajili ya kumuadhibu baba wa marehemu kwa kosa ambao wao waliliona kama kupoteza uhai wa mtu wakati uwezo wa kuchangia damu kwa rafiki yao huo walikuwa nao.

Basi bwana wale vjana wakaanza kuimba nyimbo mbali mbali zilizoashiria fujo ikiwemo ule wimbo maalumu unaotumiwa sana wakati wa ushangiliaji wa mpira na maandamano mbalimbali hua unaimbwa hivi "Ooooeeeee hoyeeeeee hoyeeee hoyeeeee ....hoyeeee hoyeeee"
Hizo ni baadhi ya nyimbo ambazo zilikuwa zikitumbuiza makaburi kabla shughuli za mazishi hazijaanza na huku mwili wa kijana wetu wa mtaani ukiwa pale pembeni ya kaburi.

Basi bwana wale vijana walipoambiwa watulie waligoma waliendelea kutumbuiza kwa singo mbalimbali ilimradi sherehe maana haikuwa msiba tena. Na walipoambiwa mmoja wao aseme wanatatizo gani Ndipo kijana mmoja akainuka na kuanza kuomba watendewe yafuatayo kabla mwili ule haujazikwa kinyume na hapo jamii nzima haitakuwa tayari kuzika na wala hawataruhusu shimo lao walilochimba liingizwe mwili huo na badala yake watalifukia ili wenye mwili wao waubebe wakatafute kaburi lingine waufukie.

Yule kijana akasema kwanza kabisa hatuna uhakika kama huyu aliomo kwenye hili sanduku ni jamaa yetu kwahiyo tunachotaka hili sanduku lifunguliwe ili tumuone na tuhakikishe kama ndio yeye, Wengine wotee wakaanza kushangilia na kelele zikaskika nyingi "Ndiooooo lazma tumuage jamaa yetu... tutaaminije kama ndio yeye"Ikabidi waruhusiwe na wakaingiza bisbis na kufungua ule mwili pale makaburini na kuanza kupita kuuaga huku wakishangilia na walipomaliza waliufunika. Na wakaendelea na kelele zao.

Walipoulizwa mbona bado mnaendelea na kelee wakati mnalotaka tumeshalifanya ... Tutamaliza kazi hii saa ngapi? Wakasema bado kuna maswala wanahitaji yafanyike kabla ya kila kitu kuendelea pale.
"Hapa hakuna kinachoendelea mpaka baba wa marehemu aje hapa mbele kuna maswali tunataka kumuuliza" mmoja wa vijana alisema huku wenzake wote wakawa wanashangilia ndipo mwenyekiti wa kijijiji alipo waomba wale vijana watulie yule mzee akaitwa. Yule baba wa marehemu akaambiwa aje pale mbele ...akatokea akiwa ametinga suti moja kali hivi huku kajitai kalikoenda chuo maana nikisema kalikoenda shule katakuwa sio kazuri sana.
Basi akasimama pale mbele ya lile sanduku lenye ule mwili huku akiwatazama wale vijana na kusubiri maswali.

itaendelea katika sehemu ya pili
aamsuni

0 comments