Saturday, July 9, 2011

Lengo la Kuumbwa Mbingu, Ardhi na Vilivyomo. 1. 1

Mbingu, ardhi na vyote vilivyomo avikuja kwa baati mbaya bali vimeubwa, na aliyeviumba si mwingine bali ni Allah (s.w) kama Qur'an inavyotueleza.
"Hakika Mola mlezi wenu ni Mwenyezi Mungu aliyeziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Kisha akatawala juu ya kiti cha Enzi......." (7:54)

Na pia anasema katika Qur'an tukufu " Yeye ndiye aliyekuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi. Tena akazielekea mbingu na akazifanya mbingu saba. Naye ndiye mjuzi wa kila kitu" (2:29).

Ni ngumu kutengeneza kitu bila kukiwekea kazi ama maleng yake. Hivyo hivyo kwa Mola mlezi aliyeumba mbingu na ardhi na vyote vilivyomo kaviwekea malengo ama kazi yake.

Tukirejea kwenye Qur'an tunakutana na aya mbali mbali zinazo zungumzia lengo la kumbwa vitu hivyo. "Na amefanya ukutumikieni usiku na mchana, na jua na mwezi, na nyota zikutumikieni kwa amri yake. Hakika katika hayo zipo ishara kwa watu wenye akili. Na hivi alivyo vieneza katika ardhi vya rangi mbalimbali. Hakika katika hayo ipo ishara kwa watu wanao waidhika. Yeye ndiye aliyeifanya bahari ikutumikieni, ili kutokana na humo mpate kula nyama laini na mtoe humo mapambo mnayo yavaa. Na unaona marikebu zikikata maji humo, ili mtafute fadhila yake na mpate kushukuru na kaweka katika ardhi milima ili ardhi isiyumbe yumbe nanyi. Na mito, na njia iti mupate kuongoka. Na alama nyengine na kwa nyota wao wanajiongoza." (16: 12-16)

"Na amefanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, vyote vimetoka kwake. Hakika katika hayo zimo ishara kwa watu wanao fikiri." (45:13).
"Yeye ndiye aliye idhalilisha ardhi kwa faida yenu, basi tembeeni katika pande zake, na kuleni katika riziki zake. Na kwake yeye ndio kufufuliwa." (67:15)

Kutokana na aya hizo tunaona kuwa kuumbwa kwa mbingu ardhi na vilivyomo ni kwa malengo makuu mawili nayo ni; Kuonyesha ishara kwa wale wenye kutafakali na kumtumikia binadamu.

0 comments