Sunday, July 17, 2011

Ajiua kwa kifo cha mkewe

NICHOLAUS Maleko (43) mkazi wa Boko, amejiua kwa kunywa sumu baada ya mke wake Catherine George [25] kufariki kwa kile kilichodaiwa ni kunywa pombe wakati akiwa kwenye dozi.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema kuwa marehemu Maleko alifariki kwa kunywa sumu baada ya kukuta mwili wa mke wake chumbani ukiwa umekufu. Kamanda Kenyela alisema marehemu Maleko kabla ya kifo chake aliacha ujumbe uliosema uamuzi huo ameupata baada ya kukuta mke wake waliyefunga nae ndoa miezi sita iliyopita kumkuta chumbani akiwa amekufa.

Ujumbe huo ulisema mke wake alikuwa ni mwanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na kujisikia huzuni baada ya kukuta mwili huo ukiwa na chupa za bia pembeni alizokuwa amekunywa Marehemu Catherine ilidaiwa kuwa alikuwa akiendelea na dozi ya ugonjwa ambao ulikuwa haujafahamika na kuhisiwa huenda bia hizo ndizo zilizosababisha kifo chake.

Maiti zote zimehifadhiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Taarifa ya Jostina Justus

0 comments