Baada ya kukutana na blog ya Bonde FC ilinibidi niitembelee timu hiyo inayo undwa na wachezaji wenye umri chini ya miaka 21 iliyopo Mwanyamala Kisiwani.
Nilifunga safari kutoka maskani kwangu Mikocheni mpaka Mwanyamala Kisiwani kuwatazama vijana hao wa Bonde FC, japo kuwa sikuwahi kufika mahali hapo lakini nilifanikiwa kufika na kukuta vijana wakifanya mazoezi.
Mazoezi ya leo yalikuwa na mahudhurio madogo huku wachezaji wakifanya mazoezi katika makundi mawili ya wachezaji ambapo kundi moja lilikuwa wenye umri chini ya miaka 16 na lingine kuondwa na wale wenye chini ya miaka 21, huku kukiwa na watoto wadogo wakicheza mpira pembeni yao.
Kilicho nivutia zaidi ni namna timu changa kama hiyo inavyomiliki blog wakati timu za ligi kuu Tanzania Bara wakipuuzia suala la kuwa na tovuti katika mtandao. Nnje ya hapo nikiwanja wanacho tumia kufanya mazoezi ambacho ni kibovu kupita maelezo.
Timu ya Bonde FC inaitaji michango ya wadau wa mpira katika kufikia malengo yao, ikiwa pamoja na kuukarabati uwanja wao ulio haribiwa na mvua na kupelekea kushindwa kufanya mazoezi ya uwanja mzima.
Pamoja na kuwa na uwanja mbovu ambao unawanyima uhuru wachezaji wa Bonde FC lakini walifanikiwa kuishia hatua ya Robo Fainali katika michuano ya DAYOSA chini ya miaka 20 nakutoa wachezaji watatu katika kikosi cha mkoa.

0 comments