Monday, August 22, 2011

Jawabu Kati

Katikati ni kati, bayazuri ni kati, twakwimu ni kati, twatafuta kati, mbora aliye kati, hakutwa na msatiri, jawabu langu ni kati, uniulizapo swali,

mjanja hukaa kati, uovu wake kufichwa, kipimo sahihi ni kati, hupatikana kwa kugawanya, ukishindwa kufika kati, mtihani utarudia, jawabu langu ni kati, uniulizapo swali,

ushindi uko kati, makocha wote hukimbilia, wagombania kati, kustarehe juu ya kitanda, sauti ya kati, tamu kusikiliza, jawabu langu ni kati, swali uniulizapo,

nikisema kizuri, kwa wengine kinanuka, kutafakari nime tafakari, jawabu lipi linafaa, lisilopeleka hasidi, majigambo kukata tamaa, jawabu langu ni jati, huniulizapo swali,

kati popote hupatikana, rahisi kupata tiki, sikwamba na bahatisha, jawabu langu sahihi, popote husimama, kwenye mapenzi na dini, jawabu langu ni kati, pale uniulizapo swali,

ibada ikipungua, hukupeleka kwenye ufakiri, hukizidisha ibada, hukupeleka kwenye shiriki, ubara wa ibada, ni kufanya kati, jawabu langu ni kati, uniulizapo swali,

kupenda nitapenda, kamwe sitovuka kati, haki kukupatia, kwa kuwa niko kati, dhuluma sitaki tenda, nasimama kati, jawabu langu ni kati, uniulizapo swali,

0 comments