Thursday, August 18, 2011

Kumi la kuachwa huru liko njiani

Asalaam alaykum warahmatullah wabarakatuh.
Natumai wasomaji wangu wote ni wazima wa Afya na mnaendelea vyema na Funga kwa wale wenye kufunga, huku pilika pilika zikienda vyema.

Hivi sasa tunaelekea ukingoni mwa kumi la pili la mwezi wa Ramadhani ambalo Allah (s.w) anawasamehe waja wake. Tunaomba kwa Allah (s.w) tuwemiongoni mwa waja tulio bahatika kusamehewa katika kumi hili la Maghfira.

Tunamalizia kumi la pili ndipo tulianze kumi la tatu, ambalo ndilo linapatikana usiku ulio teremshwa Qur an Karim. Usiku wa Laylatul qadir unapatikana katika kumi la mwisho wa Ramadhani ambao ndio usiku uliotukuka na Qur an kuteremshwa.

Usiku wa laylatul Qadir anao utambua ni Allah (s.w) pekee na hivyo kuwa sunna kwa waislam kuutafuta kwa kuongeza ibada katika kumi la mwisho, hususani katika tarehe ambazo hazigawanyiki kwa mbili yaani 21, 23, 25, 27 na 29.

Usiku huo ubora wake ni zaidi ya miezi 1000. Na ukikukuta kwenye ibada unahesabiwa umefanya ibada kwa kipindi cha miezi 1000.

Ndani ya kumi la mwisho waja huwachwa huru na Moto. Allah (s.w) huwaondolea waja wake adhabu ya moto katika maisha baada ya kufa.

0 comments