Tukio la kujitoa muhanga nusura litokee hii leo katika jengo la PPF-House jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa taarifa zilizowekwa na watu katika mitandao ya kijamii ya Jamii Forum ambako ninakutana na Bei Mbaya pamoja na Facebook ambako na kutana Anthony Mtaka Chiganga wanasema:
Bei Mbaya: Nikiwa nafatilia hati hapa manispaa ya ilala ghafla polisi wakiwa na magari na pikipiki wanafika na kuondoa wafanyakazi na waliomo kwa taarifa za kiinteligensia kuna mtu anataka kujilipua na mabomu
Anthony Mtaka Chiganga: BREAKING NEWZ-DUH-OFISI JIRANI NA KIBANDA NACHOUZIA MAHINDI YAHISIWA KUINGILIWA NA NINJA MWENYE BOMU LA KUJILIPUA, WATU WASHUKA GOROFA ZAIDI YA KUMI KWA KUKIMBIA BILA LIFT, TAHARUKI KUBWA YATOKEA!!! PPF-HOUSE-DAR!!!
Bei Mbaya: Inadaiwa alifatiliwa tokea wizarani. akimsubiri mkurugenzi. ni mmama kagoma kutoka na mabegi yake yanahofiwa kuwa na mabomu kwani sensor inalia
Bei Mbaya: ffu wamemtoa kwa mwonekano ni mwanamke, kavaa hijbu kajikandika malipustic na mawanja na mabegi mawili. anaonekana hana wasiwasi. wanadai muuza nguo, alimsubiri mkurugenzi masaa 3. askari wengine ofisi ya mkuu wa mkoa.
Anthony Mtaka Chiganga: VYOMBO VYA THIBITISHA HALI NI SHWARI-WATU WAREJEA MAOFISINI KUENDELEA NA KAZI, NAMI NAENDELEA KUCHOMA MAHINDI KWA WADAU!!!



0 comments