Friday, September 9, 2011

Kufuatia vifo vya wachezaji, wengine 30 wajitokeza kuunda timu mpya

Siku chache baada ya kutokea ajali ya ndege ambayo imeangamiza wachezaji 36 wa timu ya mpira wa magongo kwenye barafu ijulikanayo kama Lokomotiv Yaroslavi, imefahamika jumla ya wachezaji 30 wamejitokeza kuunda timu mpya Chama cha mchezo wa mpira wa magongo nchini Urusi kimetoa wito kwa vilabu vyote 18 vinavyoshiriki ligi ya mchezo huo kuwaruhusu wachezaji 3 kuhamia kuunda timu hiyo mpya.

Mtendaji mkuu wa chama cha mpira wa magongo, Vya cheslav Fetisov amesema pamoja na klabu ya Lokomtiv Yaroslavi kupewa nafasi ya kuwapandisha wachezaji wake wa timu ya vijana bado wanahitaji nguvu ya wale wazoefu ili waweze kushiriki ligi hiyo.

Wachezaji wengi wameonesha kujiunga na timu hiyo mara baada ya tarifa hiyo na kinachofanyika sasa ni jopo la ufundi kuchagua wachezaji watakao weza kuziba nafasi zilizowazi.

Ni mchezaji wa nafasi ya winga, Aleksandr Galimov ambaye amenusurika lakini hali yake ikiwa mbaya kutokana na kuungua asalimia themanini pamoja na injinia wa ndege hiyo aina ya Yak-42 Aleksandr Sizov.


Startvtz.com

0 comments