Sunday, November 6, 2011

Allahu akbar, zarindima Dar



Allahu akbar, Allahu Akbar, ndiyo maneno yaliyokuwa yanasikika asubuhi ya leo katika maeneo mbalimbali ya Jijini Dar es salaam na Tanzania nzima kwa ujumla, ikiwa ni ishara ya kuwa Waislam wako kwenye siku ya Eiddil ambapo husheherekea kwa kumaliza ibada husika.

Leo dhulhija 10 ambapo mahujaji hukamilisha ibada ya Hijja kwa kunjinja na wale ambao hawakupata fursa ya kuhiji hujumuika nao kwa kusheherekea pamoja na kunjinja wanyama halali kunjinjwa katika siku ya leo.

Waislamu wa Tanzania waliungana na ndugu zao ulimwenguni kwa kuhudhuria Ibada ya Swala ya Eiddil Adh-ha katika misikiti na viwanja mbalimbali.

Mtandao wa Aboodmsuni ulikuwa katika viwanja vya Jangwani ambapo kama kawaida viliswaliwa swala ya Eiddi hapo.

Swala ya Eidi huenda sambamba na khutuba ambapo mukhutubiaji aligusia swala la Ushoga huku akitoa tahadhari kwa kupitisha jambo hilo yanayoweza kuikumba Tanzania, akiambatanisha kisa cha Nabii Luti ambao watu wake walikubuu katika ushoga na hatimaye kuangamizwa vibaya.

Mukhutubiaji vile vile alisema vitisho vya kiuchumi ni kawaida ya makafiri kuviweka pale wanapotaka jambo lao kufanyika, kwa kutoa visa vifupi vilivyo wakumba Mitume na waumini wake.

0 comments