WACHEZAJI gofu tisa kutoka Kenya wakiwepo wa timu ya taifa ya nchi hiyo wamethibitisha kushiriki michuano ya mwaka huu ya Tanzania Open.
Michuano hiyo ya siku nne ya viwanja 72 imepangwa kuanza kesho hadi Jumapili kwenye Viwanja vya Klabu ya Gymkhana Arusha.
Akizungumza na HABARILEO mjini Dar es Salaam, Ofisa Tawala wa Chama cha Gofu Tanzania (TGU), Sophie Nyanjera alisema maandalizi yanakwenda vema.
“Kenya amethibitisha kuleta wachezaji 9 kwenye Tanzania Open,” alisema. Michuano hiyo ya
mwaka huu kwa mujibu wa Nyanjera inadhaminiwa na bia ya Tusker Malt na zaidi ya wachezaji 100 wanatarajia kushiriki.
Alisema michuano hiyo ambayo wachezaji watawania pointi za order of merit itakuwa ya viwanja 72. Michuano hiyo pia itatumika kama maandalizi kwa wachezaji wa taifa kabla ya Kombe la Challenge Afrika Mashariki ambayo imepangwa kuanza Novemba 8 hadi 11 kwenye viwanja hivyo ikishirikisha timu kutoka nchi tano Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na wenyeji Tanzania.
Ofisa huyo alisema pia kuna makundi ya waalikwa ambao ni wanaume wenye kiwango cha mchezo huo kuanzia handicap 10 hadi 18 na wanawake kuanzia handicap 24 na kushuka.
Nyanjera alisema kundi hilo la waalikwa kwa upande wao watachuana katika viwanja 36 kwa siku mbili (Jumamosi na Jumapili).
Habari leo
0 comments