Thursday, December 1, 2011

Msaada Tutani: Tunaadhimisha miaka 50 ya uhuru wa TANGANYIKA ama wa TANZANIA?

Kuuliza si ujinga, na si kila mzungumzaji anajua anacho zungumza. Nimekuja na swali ambalo lina nitatiza, si mimi tu, najuwa wako wengine pia wengi. TANZANIA IMEPATA UHURU LINI?

Hili swali limejengeka baada ya mwendelezo ya maneno yanayotajwa na vyombo vya habari vyote nchini ambapo husema "tunaelekea katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania."

Kwa elimu yangu ndogo niliyojaaliwa na Mola, inaniambia TANZANIA ilizaliwa mwaka 1964 ambapo ni miaka 46 iliyopita kufuatiwa muunganisho wa TAN (Tanganyika) na ZAN (Zanzibar).

Kwa elimu yangu hiyo ndogo inaniambia Tanganyika imepata uhuru wake mwaka 1961 december 9, ambapo ni miaka 50 iliyopita.

Wakubwa naomba jawabu, tunasheherekea miaka 50 ya Uhuru wa TANZANIA, ama wa TANGANYIKA. Niwekeni sawa katika matumizi ya majina hayo.


Natoka huko kwa wanasiasa na rejea TFF (Shirikisho la mpira wa miguu nchini) na wadau wa mchezo wa Soka waniweke sawa katika hili.

Katika michuano ya CECAFA tumepata kushuhudi timu ya ZANZIBAR ikitumia jezi zao, wakati ya TANZANIA BARA (Kilimanjaro Stars) wakitumia jezi za timu ya Taifa ya Mungano (TAIFA STARS) hapa pamekaaje wakubwa.

Naombeni msaada.

0 comments