Thursday, December 29, 2011

Msuni arejea Bongo


Msuni


Blogger Abdallah Hamdun Sulayman 'Aboodmsuni' anaye fanya kazi zake katika Aboodmsuni Na Soka La Bongo, Aboodmsuni Home na Azam Fans Club anatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam 'Bongo' hii leo teyari kwa kurejea skonga jumatatu ya january 2.

Msuni alikuwa mkoani Morogoro katika kambi ya chuo kikuu cha waislam Morogoro, ambapo alikuwa ana kula likizo yake ya mwezi mmoja na nusu, ambayo inaelekea ukingoni.

Akiwa Morogoro kama ilivyo ada alipata fursa ya kurejea uwanjani na kucheza mechi mbili ambapo zote timu yake ya wafanyakazi wa chuo cha kiislamu Morogoro walipoteza. Huku timu yake ya mtaa inayotambulika kwa jina la Cosovo ama Eleven Boys alikuta imesambaratika na kukuta madogo (u14) wakiwa wanapewa makali na kocha wa timu hiyo Kabunda.

0 comments