Mvua za kufunga mwaka zinazoendele pande mbalimbali za nchi, zimeshatoa madhara katika kona mbalimbali za Jiji la Dar es salaam.
Kwa mujibu wa taarifa zilozoufikia mtandao huo, zinasema kuwa cheche za umeme zimeshuhudiwa sehemu mbalimbali za jiji huku zikimkomba Mtoto mmoja, wakati maeneo ya Mbagala kukiwa na hatihati ya nyumba kuwaka moto kufuatia na cheche hizo.

Eneo la mto wa Kigogo ambao umefurika na kuwaweka katika wakati mgumu watu wenye makazi yanayo zunguka mto huo, ambapo kuna uokozi unaendelea, huku gari lililokuwa limeegeshwa kando ya mti likiangukiwa na mti huo.
Njia ya mkato ya kutokea Ubungo kwenda Chuo kikuu imesitisha huduma kufuatiwa daraja lake kuharibiwa na mvu, huku kukiwa na taarifa ya mzee kuchukuliwa na maji.
0 comments