Fatma Said,
Zanzibar
PAZIA la Mashindano ya Kombe la Mapinduzi kwa mchezo wa netiboli linafunguliwa leo Zanzibar kwa mchezo kati ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Queens’ na timu ya Taifa ya Uganda.
Mashindano hayo yanashirikisha nchi sita na yatakuwa yakichezwa Uwanja wa Gymkhana mjini hapa.
Katika mchezo huo wa ufunguzi mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Makazi, Ardhi, Maji na Nishati Ali Juma Shamuhuna saa kumi alasiri.
Akizungumza na gazeti hili Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Zanzibar (Chaneza), Rahima Yussuf alisema timu zote shiriki zilitarajiwa kuwasili jana.
Alizitaja timu nyingine zitakazoshiriki kuwa ni Zambia, Zimbabwe, Msumbiji, Kenya na Uganda.
Friday, January 6, 2012
Related Post
0 comments