Tuesday, January 31, 2012

Nchi ya migomo, wakutetea haki wakitunisha mifuko yao

Tanzania, Tanzania nchi ya mababu zangu, haindeshwi bila migomo, kila mtu hula kwa urefu wa kamba yake, bila kujali athari ya wachini yake.

Mwaka jana foleni zilihamia vituo vya kuuzia mafuta, mwaka huu wagonjwa wakosa huduma mahospitalini, wakati wazee wakugonga meza wakitunisha mifuko yao.

Wakiwapuuzia madaktari, huku mahospitalini wagonjwa wakiwa katika hali tete. Huku wakidai hali ngumu Dodoma, hivyo kutunisha mifuko yao.

Hii ndio Tanzania leo Madaktari, kesho walimu, keshokutwa wanafunzi wa vyuo, mtondogoo wauza mafuta, kisha wasafirishaji, huku wao wakitunisha mifuko yao huku hali inazidi kuwa ngumu kwa Mtanzania kwa vitu kupanda bei.

0 comments