Thursday, January 26, 2012

Simulizi: Mwalimu atoa darasa kwa wazazi kupitia Mtoto na kifo cha rafiki wa Mzazi

Kuna mwalimu mmoja alikuwa akifundisha wanafunzi wa darasa la tatu.

Katika moja ya vipindi vyake mwalimu huyu, siku moja katika kusherehesha darsa akazungumzia swala ya alfajiri. Alikuwa akizungumza kwa usulubu wenye kuathiri sana. Akazungumzia umuhimu wa swala ya alfajiri na fadhila zake.

Katika wanafunzi wale wa darasa la tatu kuna mwanafunzi aliathirika Sana na yele mazungumzo, kwani mwanafunzi huyo alikuwa hajawahi swali swala ya alfajiri wala jamaa zake wa nyumbani kwake.

Pindi alipo rudi nyumbani alifikiri sana! Afanye nini ili aweze amka wakati wa swala ya alfajiri? Hakupata suluhisho isipokuwa kukesha usiku mzima ili aweze Swali swala ya alfajiri.

Akafanikisha kuteleleza azma yake ya kukesha, lakini likajitokeza tatizo! Msikiti msikitini ni mbali, na hawezi elekea peke yake!!!

Ghafra akasikia sauti ya viatu nje, akafungua mlango haraka. Akamuona mtu aliye kuwa akielekea msikitini, alikuwa ni babu wa rafiki yake Ahmadi jirani yao.

Yule mtoto wa darasa la tatu akamfuata yule mzee nyuma nyuma kwa kujificha ili asije akagundua na kuwaeleza familia yake.

Hali ikaendelea hivi hivi siku zote, akielekea msikitini swala alfajiri kwa kujificha. Lakini kudumu hali ni muhali, kwani alifariki yule mzee, babu wa rafiki yake Ahmadi.

Pindi yule mtoto alipo jua ya kwamba yule babu kafariki, alilia sana!!! Wazazi wake wakashangaa!!!

Baba yake akamuuliza: Mwanangu kwa nini walia kiasi hiki, Hali ya kuwa aliye fariki si rika lako, ili uweze cheza nae?! Na wala si ndugu yako wa nyumbani unaye weza mkumbuka?!

Yule mtoto akamuangalia baba yake kwa macho yenye kutokwa na machozi Na kwa mtizamo wa huzuni!.

Kisha akasema: Natamani aliye fariki ungekuwa ni wewe na wala si yeye!.

Baba akashtushwa kwa lile jibu, akajiuliza kwa nini mwanangu ananijibu hivi na kwa usulubu huu???! Kwa sababu gani mwanangu anampenda mzee huyu kiasi hiki???!

Kisha yule mtoto akaendelea kumweleza baba yake ya kwamba, mie sisikitiki na kupatwa na uchungu kwa sababu hizo unazo zitaja.

Baba akashangaa!!! Akamuuliza tena, kwa hiyo walia kwa sababu gani?

Akamjibu: kwa sababu ya swala. Kisha akaanza kufuta machozi na kumuuliza baba yake, Baba kwa nini huswali swala ya alfajiri? Kwa nini baba hauwi kama yule babu na kama walivyo watu wengi nilio waona?

Baba akashangaa, akamuuliza: Umewaona wapi???

Mtoto akajibu: Msikitini.

Baba akauliza: umewaona vipi???

Akamsimulia jinsi ilivyokuwa.

Baba akaathiriwa sana na mwanae, machozi yakamdondoka! Akamkumbatia mwanae.

Na toka siku ile hajawahi kosa swala yoyote msikitini.


MIMI NI MUISLAM

0 comments