Sunday, January 15, 2012

Wakati wakuchagua Taifa


Mwezi wa kwanza kama ilivyo namba moja kuipata ilivyokuwa ngumu ndivyo hivyo hivyo ulivyo mwezi huo, ambao wengine huita mwezi wa mifuko kutoboka.

Mwezi wa kwanza huwa ni mwezi unaowapa presha wahitimu wa kidato cha 4, wakati wanafunzi wa kidato cha 6 wakikusanya silaha za kuikabili mitihani wataifa huku madenti wengine wakirejea mashuleni wakiwa na shauku ya kujua nini kilichopo katika darasa lao jipya.

Katika ulimwengu wa soka la bongo ni wakati wakupika fitina za namna ya kumngoa aliye kileleni na wa kileleni ni namna ya kubaki kileleni.

Kwenye soka la ukweli lenye mashabiki wengi ni wakati wa makocha kufanya vitu viwili kwa wakati mmoja (usajili na muendelezo wa ligi) huku mashabiki wakiwa na hamu ya kujua nani anaongezwa kwenye vikosi vyao na nani anaondoka, huku wakiwa na shauku ya kushuhudia ushindi kila timu yake inapoteremka.

Kila baada ya miaka miwili barani Afrika kunakuwa na mashindano ya Mataifa ya Africa 'AFCON' ambapo mara ya mwisho Tanzania kushiriki ilikuwa mwaka 1980 nchini Nigeria.

Ikiwa imebaki masiku kadhaa kipute cha Mataifa ya Afrika nchini Equateria Guinea, ni wakati wa mashabiki wa soka toka Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki kuchagua mataifa ya kushangilia.

Kipute cha ufunguzi kitakuwa GUINEA EQ. vs. LIBYA january 21 ikifuatiwa na SENEGAL vs. ZAMBIA.

Michezo mingine ya awali itakuwa;
22/01/2012
COTE D’IVOIRE vs. SUDAN
BURKINA FASO vs. ANGOLA
23/01/2012
GABON vs. NIGER
MOROCCO vs. TUNISIA
24/01/2012
GHANA vs. BOTSWANA
MALI vs. GUINEA
25/01/2012
LIBYA vs. ZAMBIA
GUINEA EQ. vs. SENEGAL
26/01/2012
SUDAN vs. ANGOLA
COTE D’IVOIRE vs. BURKINA FASO
27/01/2012
NIGER vs. TUNISIA
GABON vs. MOROCCO

0 comments