Monday, April 25, 2011

Kunahaja ya kuwa na serikali 3

aamsuni:

Tukiwa tunaelekea katika maadhimisho ya miaka 47 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar hapo kesho tarehe 26 april, kuna baadhi ya mambo lazima yaangaliwe yasije vunja muungano au kutuingiza kwenye vita.
Kuna mambo mengi sana ila mie ningependa kulizungumzi hii ya kuwa na serikali mbili baadala ya tatu au moja. Ni ngumu kumuelewesha mtu kuwa kuna muungano wa Zanzibar na Tanganyika (Tanzania bara) wakati kuna serikali mbili, serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na serikali ya Muungano.
Wakati nipo kidato cha pili nilikuwa nali kosa swali la kuchagua ambalo linazungumzia jamhuri ya muungano ya Tanzania ina serikali ngapi. Maana jawabu la mbili ambalo ndio sahihi aingii akilini.
Kutokana na kuto ingia akilini kwa oja ya kuwa na serikali mbili ina kuwa rahisi mtu mwenye dhamira ya kuvunja muungano huu kufanikiwa, kwa kuwa inaonyesha dhairi kuwa si muungano wa kutekeleza haki na usawa katika kila upande za muungano huu.
Unaweza kujiuliza ni serikali ipi inayosimamia mambo ya Tanzania bara (Tanganyika) ambayo hayamo katika muungano kama michezo, nishati na mengineyo. Ni ngumu kuniambia serikali ya muungano ndiyo isimamie mambo ya Tanzania bara na Zanzibar bila kuweka upendeleo upande wake.

Hili suala ndilo linalo waumiza vichwa Tff na CHANETA kwa kusimamia michezo hiyo katika picha ya muungano na picha ya kitanzania bara.
Huu muungano wa serikali mbili ni danganya toto ya kukuletea zawadi huku ukirudi mikono mitupu.
Ni wakati wa serikali kuliangalia hili suala la kuwa na serikali 3 kwa kuepusha migogoro inayoweza kuibuka hapo mbele wananchi watakapo amua kukomesha dhulma. Moja ya sababu iliyopeleka machafuko Sudan na kujigawa ni hili la kupendelea upande mmoja.
Ni ngumu kwa serikali yetu ya muungano kutenda haki kwa pande zote mbili kwa kuwa inacheza na majukumu mawili tofauti nayo ni kusimamia Tanzania bara pamoja naTanzania kwa ujumla. Kama mmeweza kuanza mchakato wa kubadili katiba na hili la kuwa na serikali 3 linawezekana kwa kuulinda muungano wetu.

HAKUNA AMANI YA KUDUMU KATIKA SEHEMU YENYE DHULMA

0 comments