Monday, May 30, 2011

Si ogopi kutendwa

Nikikumbuka nilikotoka, nabaki mdomo wazi,
natamani nirudi nyuma, nikatibuwe mikosi,
maji nisha yavulia, vipi nirejeshe mavazi,
nimeamua kupenda, vipi ni ogope kutendwa,

karibu nyumbani, nakupokea kwa furaha,
ukawaone wazazi, wenzako walivyo tenda,
historia iko wazi, wa weza isoma,
nimeamua kupenda, vipi niogope kutendwa,

kufungu mlango kawaida, hodi ikipigwa,
mapumziko utapata, ukimaliza nenda,
waweza bakia, usafishe chumba,
nimeamua kupenda, vipi niogope kutendwa,

unashangaa nini, wengi wamepita,
wamefanya mengi, machozi yasha kauka,
nimependa wengi, siwezi acha kupenda,
nimeamua kupenda, vipi ni ogope kutendwa.


aamsuni

0 comments