Thursday, August 11, 2011

Dar shwari, Mbeya bado halimbaya

Hali shwari katika jiji la Dar es salaam baada ya huduma ya mafuta kurejea katika hali yake. Lakini katika jiji la Mbeya hali ni tofauti zaidi hii leo.

Asubuhi mida ya saa 4 nilikutana na post kwenye facebook inayoelezea nauli kupanda kufika Tsh 500 kituo hadi kituo toka Tsh 300. Jioni hii nimekutana na taarifa katika blog ya michuzi ikisema nauli imefika Tsh 1000 kituo hadi kituo.

Pamoja na kupanda huko bado huduma hiyo ya daladala ni shida. Hali hiyo inatokana na mgomo walio ufanya watoa huduma ya mafuta ya kuendeshea mitambo.

0 comments