Hali si shwari maeneo ya Mbagala jijini Dar es salaam kufuatia kimbunga kikali kilicho tokea.
Tuungane na vyanzo vya habari kwa habari zaidi.
ANDREW CHALE KATIKA FACEBOOK.
Hali ya hatari mbagala....kimbunga kikali kimeezua nyumba zaidi ya 16 na nyingine kuaribiwa vibaya huku watu mbalimbali wakijeruhiwa..huko Mbagala kwa Mangaya.
Habari zinasema kua wasiwasi wao hawajui mabati yaliyoeruliwa huko yalipo imekuaje maana yalitoka mwendo mkali na wa ajabu..zaidi tutawajuza ila watu wanne wamejeruhiwa vibaya wamekimbizwa hospitali. sorce: Action Team (Tanzania Red cross- Dar es Salaam)
MICHUZI BLOG.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini imetoa ufafanuzi kufuatia Kimbunga kilichoambatana na Mvua kali na kusababisha Nyumba zaidi ya 90 kuezuliwa Mapaa yake huko Mbagala eneo la Mangaya katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa Hali ya Hewa Dokta Hamza Kaberwa ameiambia Uhuru FM leo kuwa hali hiyo ya Kimbunga inatokana na mabadiliko madogo ya Ardhi katika Bahari ya Hindi.
Kimbunga hicho kilichoambatana na Mvua pia kimesababisha watu Wanne kujeruhiwa vibaya.
Kufuatia hali hiyo imesema mabadiliko hayo yametoka Baharini kuelekea Pwani ya Dar es salaam kwa umbali wa Kilometa Mbili hadi Tano na hivyo kusababisha Kimbunga hicho kilichoambatana na Mvua.
Pamoja na mambo mengine Mamlaka hiyo ya Hali ya Hewa imetoa tahadhari kwa wananchi kuwa Mvua za Vuli zitakuwa Juu ya Wastani katika eneo la Kaskazini ikiwemo Dar es salaam hivyo wananchi wachukue tahadhari za kukabiliana na hali hiyo hususani wananchi wanaoishi Mabondeni.
Wakati huo huo, Mvua hizo pia zimesababisha Mifereji ya Maji Taka kujaa na kusababisha Maji Taka kusambaa katika barabara na maeneo kadhaa ya Jiji la Dar es salaam hatua iliyoleta usumbufu kwa wananchi.
0 comments