Siku chache baada ya kikundi cha watu waliojiita viongozi wa Baraza Kuu la Waislam (BAKWATA) wilaya ya Igunga, kutoa tamko la kuwataka Waislam wilayani hapa kutoipigia kura CHADEMA, siri imefichuka kuwa watu hao ni makada wa CCM.
Habari za uhakika kutoka katika chanzo cha kuaminika kilicho ndani ya kundi hilo zinasema kuwa kikundi hicho hakikuwa na dhamira ya kweli ya kutetea Uislam kama walivyodai mbele ya waandishi wa habari, bali kilikuwa na ajenda ya kisiasa kikitumiwa na CCM ili kuidhoofisha kisiasa CHADEMA.
Kufuatia madai hayo ya kuvuliwa hijabu, Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) wilaya ya Igunga, lilitoa tamko kulalamika na kulaani kile walichokiita kunyanyaswa na kudhalilishwa kwa mwanamke wa Kiislam, DC Kimario.
Kufuatia kutolewa kwa tamko hilo lililoonekana wazi kubeba ajenda ya kisiasa, gazeti hili lilianzisha uchunguzi wake ambao umebaini kuwa watu hao ni wanasiasa kutoka vyama vya CCM na CUF ambao baadhi yao ni viongozi wakuu hapa wilayani.
Kwa mfano, mmoja wa watu hao, Maulid Athuman Mussa, aliyejitambulisha kama katibu wa Bakwata wilaya ya Igunga imebainika kuwa ni katibu wa wilaya wa chama cha waananchi (CUF).
“Ndugu mwandishi ulikuwa sahihi kabisa uliposema walikuwa wakisukumwa na jambo lililojificha nyuma ya pazia, ukweli ni kwamba wenzetu ni wanasiasa kabisa, wengi ni makada wa CCM na yule katibu wa wilaya wa Bakwata ni katibu wa CUF, walitumiwa tu na CCM kuidhoofisha CHADEMA, wengine tulikuwepo pale kama bendera fuata upepo,” kilisema chanzo chetu hicho.
Mussa alionekana dhahiri kuwa na msukumo wa kisiasa wakati alipokuwa akisoma hicho kilichodaiwa kuwa tamko la Waislam, na ndiye aliyesababisha mkutano huo kuvurugika baada ya kukataa kujibu maswali ya waandishi wa habari.
Uchunguzi zaidi umebaini kuwa karibu watu wote waliokuwepo katika mkutano huo wa waandishi na kujitambulisha kwa nyadhifa mbalimbali za uongozi wa Bakwata wilayani hapa, ni makada wa CCM na baadhi yao wamewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi wa chama hicho wilayani hapa.
Mwandishi wetu alimfuatilia mmoja wa watu hao na kufanikiwa kupaona nyumbani kwa kada huyo wa CCM ambako ilikuwa ikipepea bendera ya chama hicho, hali inayothibitisha pasipo kuacha chembe ya shaka kuwa mtu huyo ni kada wa CCM.
Ijumaa, Septemba 23, mwaka huu, watu waliojiita viongozi wa Bakwata wilaya ya Igunga, waliitisha mkutano wa waandishi wa habari kwa lengo la kutoa tamko la kulaani kile walichodai tukio la kuvuliwa hijabu mama wa Kiislam, Fatma Kimario, ambaye ni mkuu wa wilaya ya Igunga.
Tanzania Daima

0 comments