Naibu Meya Sogere Mwakyuse akizungumza katika mahafali ya kidato cha nne kwa shule za Ununio Boys na Kunduchi girls yaliyofanyika Kunduchi alisema mzizi wa Elimu ni Mchungu wenye matunda Matamu.
Naibu meya huyo ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo yaliyo funguliwa kwa Quran tukufu iliyo somwa na Salha Adam Kaoneka muhitimu wa kidato Cha Nne.
Mgeni rasmi huyo alisema kuwa ni jitihada ndizo zinazo hitajika ili kula matunda hayo ya elimu ambayo mzizi wake ni mchungu ambao bila ya ufumilifu huwezi kuumaliza.
Katika mahafali hayo muakilishi wa wazazi walioitimu alisisitiza kwa wanafunzi kushikamana katika nidhamu.
Muakilishi huyo bwana Juma Jangila alisema kuwa wahitimu hao ni kioo katika jamii, ambapo matendo watakao fanya katika jamÃi yatatoa Taswira ya shule walizosoma. Alisisitiza pia suala zima la juhudi na kama moja ya silaha yao kwendea Mafanikioa.
Mkuu wa Shule ya Kunduchi Khadija Mgambo alizitaja changamoto zinazo ikumba shule yake pamoja na zile za kiislam katika mahafali hayo yaliyofanyika shuleni Kunduchi.
Alisema itikadi ya wazazi juu ya shule hizo za kÃislam kuwa zinafundisha Qur an na kuwafanya wazazi kushindwa kuwapeleka wanao katika shule hizo, ni moja ya changamoto wanayokabiliana nayo.
Alisema pia kuwa wanafunzi wenye uwezo mzuri hawatui shuleni hapo ama katika shule jingine za kiislam, na kupelekea Kunduchi kupokea wanafunzi wenye wastani C na kwa nadra wastani B, wakati St. Marians wanapokea wenye wastani A.
Alizungumzia pia suala la Utandawazi ambao unaifuruga jamii na kuadhili katika malezi ya watoto na hivyo kupelekea uwalimu kuwa kazi ngumu kulinganisha na huko nyuma. Vile vile aliomba ushirikiano toka kwa wazazi katika malezi ya watoto. Aligusia pia katika suala la Umeme, ambapo wanatumia jenereta lao ambalo ni ndogo na hivyo kutumiwa kwa dharura ambapo linawashwa madarasani.
Mkuu huyo aliongezea suala la Mahitajio ya Maktaba na kwa sasa wana tumia kitabu 1 kwa wanafunzi watatu, wakati dhumuni lao ni kufikia vitabu viwili kwa mwanafunzi mmoja. Pia aligusia kozi ya kompyuta kwa wanafunzi wake.
Mahafali hayo yalihudhuriwa na mkurugenzi wa Munadhamat Al Daawa Dr. Khalid Awadh akiapatana na Dr Hamdun Sulayman aliyeitumikia shirika hilo linalo simamia shule hizo, pia walikuwepo wa Bunge waliopata kusoma katika shule hizo, Muheshimiwa Rayah Khamis (aliyesoma Kunduchi) na Mbunge wa jimbo la Lindi muheshimiwa Said Mohamed (aliyesoma ununio).
Muhadhili wa Chuo kikuu cha kiislam Morogoro, Dr Hamdun akizungumza badala ya Dr Khalid aliwataka wanafunzi hao kuigwa yaliyo mema (ya kheri) na kuacha mabaya ya pite na wasiwe Monkey see Monkey Do.
0 comments